JE CHANZO CHA MWANAMKE KUTOKUBEBA MIMBA NI YEYE TU AU HATA MWANAUME?

 MIMBA

• • • • •

JE CHANZO CHA MWANAMKE KUTOKUBEBA MIMBA NI YEYE TU AU HATA MWANAUME?


Katika jamii zetu nyingi swala la kubeba mimba huwa ni la mwanamke peke yake, na hata ikifikia wakati hapati ujauzito yeye ndyo huonekana kwamba ana matatizo,


Je dhana hii ni kweli? soma hapa nikufungue macho


Sio kila mwanamke ambaye habebi mimba basi yeye ndye mwenye matatizo, kuna wanaume wengi tu ambao wana matatizo ya kiafya(afya ya uzazi) ambayo huweza kumsababisha mwanamke kutokushika mimba, mfano;


 matatizo kama kuzalisha kiwango kidogo sana cha mbegu za kiume yaani LOW SPERM COUNT, mwanaume kutokuzalisha kabsa mbegu za kiume au kuzalisha mbegu za kiume ambazo hazina ubora wowote, matatizo ya kuziba kwa mirija ya kupitisha mbegu za kiume n.k.


Matokeo ya dhana hiyo potofu, mwanamke huyu anaenda hospital anafanya vipimo vyote peke yake anaonekana yupo sawa, baba yeye anang'ang'ania tu kwamba anataka mtoto, wakati hata hakufanya kipimo chochote,


Na wakati mwingine kupelekea hadi wanandoa kuachana kisa baba anataka mtoto na mke hazai, Halafu cha ajabu anashangaa mke wake kapata mwanaume mwingine na ujauzito kabeba.


Hivo swala la kutafta mtoto katika ndoa au familia sio jukumu la mwanamke peke yake, hapa ushirikiano wa wote wawili(mwanamke na mwanaume) huhitajika, 


Maana wakati mwingine shida haipo kwa mwanamke ipo kwa mwanaume.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!