JINSI YA KUBORESHA MFUMO WA MMENG'ENYO WA CHAKULA MWILINI
CHAKULA
• • • • • •
JINSI YA KUBORESHA MFUMO WA MMENG'ENYO WA CHAKULA MWILINI
Baadhi ya mambo muhimu ya kufanya na kuzingatia ili kuboresha na kuimarisha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kwenye mwili wako,
✓ Kula zaidi matunda ambayo yana asili ya nyuzi nyuzi au Fibers kama vile; machungwa,maembe n.k
✓ Pia ulaji wa Tende, mapapai,maparachichi husaidia sana katika kurahisisha umeng'enyaji wa chakula mwilini
✓ Tafuna vizuri chakula chako, huku ukiepuka tabia ya kula chakula huku unaongea hali ambayo huweza kupelekea gesi au hewa kujaa tumboni
✓ Jenga utaratibu wa kunywa maji ya kutosha kwa siku angalau lita 2.5 mpaka 3
✓ Kula vyakula ambavyo vina kiwango kikubwa cha mafuta salama mfano; omega-3 fatty acids kama vile Samaki wakubwa,dagaa n.k
✓ Epuka msongo wa mawazo,watu wengi hawajui kwamba msongo wa mawazo huweza kuleta athari hadi kwenye mfumo mzima wa umeng'enyaji chakula mwilini
✓ Kufanya mazoezi ya mwili kila siku huboresha sana mfumo wako wa umeng'enyaji chakula mwilini
VITU AMBAVYO HUATHIRI UMENG'ENYAJI WA CHAKULA MWILINI
- Unywaji wa pombe kupita kiasi
- Uvutaji wa sigara
- Tabia ya kuchelewa sana kula chakula usiku,
pamoja na kula chakula kingi usiku halafu unaenda kulala
N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!