KWANINI WAGONJWA WA ASTHMA HUTESEKA ZAIDI WAKATI WA USIKU?(Nocturnal asthma)
ASTHMA
• • • • •
KWANINI WAGONJWA WA ASTHMA HUTESEKA ZAIDI WAKATI WA USIKU?
Tafiti zinaonyesha kwamba wagonjwa wengi wa Asthma hupata shida zaidi wakati wa usiku, na hata asilimia kubwa ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Asthma hutokea wakati wa usiku.
Mpaka sasa hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo imegundulika kuwa chanzo kikuu cha ugonjwa wa Asthma kusumbua zaidi wakati wa usiku,
Ila zipo baadhi ya sababu ambazo zimeonekana kuongeza uwezekano wa wagonjwa wa Asthma kupata shida zaidi wakati wa usiku, Na sababu hizo ni kama vile;
- Ongezeko la uzalishaji wa vichocheo vya mwili kama vile histamine hutokea wakati wa usiku ambavyo huziba njia ya hewa
- kupungua kwa kichocheo(hormones) cha epinephrine wakati wa usku ambacho husaidia katika kutanua njia ya hewa
- Kulala tu hubadilisha mfumo wa upumuaji hasa Reclining position
- Mtu kuvuta na kutoa hewa yenye ubaridi zaidi wakati wa usiku, pamoja na mazingira ya ubaridi ambao upo usiku tofauti na mchana
- Ongezeko la uzalishaji wa Mucus wakati wa usiku, ambapo huweza kuziba au kupunguza kiwango cha hewa kuingia na kutoka
- Kulala na msongo wa mawazo
- Kuwa kwenye hali ya kupatwa na Vumbi zaidi wakati umelala
MATIBABU
Hakuna matibabu maalumu kwa ajili ya asthma wakati wa usiku yaani Nocturnal Asthma,matibabu ni yale yale ambayo mgonjwa hupata siku zote
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!