MADHARA YA MAZIWA YA KOPO YA FORMULA KWA WATOTO

 MAZIWA

• • • • •

MADHARA YA MAZIWA YA KOPO YA FORMULA KWA WATOTO


Katika hali ya kawaida,mtoto baada ya kuzaliwa anatakiwa anyonye maziwa ya mama peke yake bila kupewa kitu kingine chochote kwa kipindi cha Miezi sita(6),


ambapo kwa kitaalam tunaita EXCLUSIVE BREASTFEEDING,


Lakini kuna baadhi ya wakina mama baada ya kuzaa watoto hupata changamoto ya maziwa kutokutoka, hivo kuwalazimu wengine kutumia maziwa ya Kopo,


Hata hivo wataalam wa afya huendelea kuwaelimisha na kuwasisitiza wakina mama wenye changamoto hii ya maziwa kutokutoka baada ya kujifungua, kwamba hali hii huisha na maziwa ya mama hutoka kwa kadri mtoto anavyojitahidi kunyonya,


Hivo maziwa ya kopo huwa ni ya dharura tu lakini sio ya kuyategemea kwa ajili ya kumlisha mtoto wako.


MADHARA YA MAZIWA YA KOPO YA FORMULA KWA WATOTO


- watalaam wa Afya na baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba,maziwa haya ya Kopo au FORMULA sio salama kwa watoto wadogo endapo yatakuwa ndyo Tegemezi lao, Hasa pale mama akiacha kabsa kumnyonyesha mtoto na kumpa maziwa ya kopo.


Baadhi ya madhara ambayo huweza kutokea endapo mtoto hutumia maziwa ya Kopo ni pamoja na;


1. Mtoto kushambuliwa kwa urahisi na magonjwa kwenye mfumo wa chakula na kuleta madhara mbali mbali kama vile; Gastroenteritis


2. Mtoto kupatwa na tatizo la kuharisha mara kwa mara


3. Mtoto kuwa katika hatari ya kupatwa na Kisukari hasa TYPE 1 Diabetes


4. Tatizo la Asthma


5. Vifo vya gafla kwa watoto yaani Sudden Infant Death syndrome


6. Mtoto kupatwa na maambukizi kwenye mfumo wa hewa yaani Lower respiratory tract Infection


7. Mtoto kupatwa na magonjwa mbali mbali ya ngozi kama vile; Atopic Dermatitis

N.K


KWA UJUMLA ni kwamba,maziwa ya mama humpa mtoto kinga ya kutosha dhidi ya Magonjwa mbali mbali hasa ile miezi mitatu(3) ya mwanzoni,ambapo bado mtoto hana kinga tegemezi inayotokana na mwili wake.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!