BLOOD GROUP O
• • • • • •
MAMBO YAKUFAHAMU KWA MTU MWENYE BLOOD GROUP O
1. Blood group O imegawanyika mara mbili;
- kuna O+ ikiwa na maana ya Blood group O rhesus factor POSITIVE
- Na O- ikiwa na maana ya Blood group O rhesus factor NEGATIVE
2. Mtu mwenye Blood group O ni Universal Donor;
- Ikiwa na maana kwamba, mtu mwenye blood group O rhesus factor POSITIVE anaweza kumchangia mtu mwingine yeyote damu mwenye kundi lolote la damu Rhesus factor positive, mfano; A+,B+,Ab+ na O+
- Na mtu mwenye blood group O- anaweza kumchangia mtu yeyote damu mwenye Rhesus factor POSITIVE na mwenye Rhesus factor NEGATIVE,
Hapa namaanisha kama wewe una kundi lingine lolote la damu mfano; A+,A-,B+,B-, AB+,AB-,O+,O- na unahitaji kuchangiwa damu,basi mtu mwenye kundi hili la O- anaweza kukusaidia
• Kama hujaelewa vizuri tazama blood group O hapo kwenye chart, yeye akiwa kama Donor(mchangiaji)
3. Mtu mwenye Blood group O- (recipient) huweza kuchangiwa damu na mtu mwenye Blood group O- mwenzake tu basi, yeye hawezi kuchangiwa damu na mtu mwingine yoyote zaidi ya O- mwenzake.
Na mtu mwenye Blood group O+ (recipient) yeye huweza kuchangiwa damu na mtu mwenye Blood group O- pamoja na mtu mwenye Blood group O+ kama yake.
4. Blood group O, ndiyo kundi la damu ambalo hupatikana sana kwa watu wengi zaidi, kwa ujumla wake bila kuangalia Rhesus factors(Yaani Positive na Negative)
5. Watu wenye Blood group O hushambuliwa kwa kiasi kidogo sana na Magonjwa ya moyo kama Coronary Heart disease ikilinganishwa na makundi mengine ya Damu,
Japo pia baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba watu wenye blood group O ndyo hushambuliwa na magonjwa mengine yanayohusu Bacteria au Virusi kwa kiasi kikibwa kuliko wengine ikiwa ni pamoja na matatizo kama vidonda vya tumbo
N.K
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!