gastric trichobezoar
• • • • •
UGONJWA WA NYWELE KUKUSANYIKA TUMBONI(gastric trichobezoar)
Gastric trichobezoar ni tatizo ambalo huhusisha kukusanyika kwa kiwango kikubwa cha nywele ambazo hazikufanyiwa umeng'enyaji kwenye mfumo wa chakula katika maeneo mbali mbali ya mfumo huu wa chakula kama vile; Tumboni n.k
CHANZO CHA TATIZO HILI LA gastric trichobezoar
- Tatizo hili la mtu kuwa na kiwango kikubwa cha nywele kukusanyika tumboni huchangiwa kwa asilimia kubwa na Mtu kula nywele mara kwa mara, kwa kiwango kikubwa na ndani ya muda flani,
Tatizo hili huwapata sana watu wenye matatizo ya akili ambao hupenda kula vitu vichafu sana ikiwa ni pamoja na kula nywele kwa kiwango kikubwa sana
WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA TATIZO HILI
✓ wenye matatizo ya akili
✓ Waliofanyiwa upasuaji unaohusu mfumo wa chakula
✓ Wenye magonjwa ambayo husababisha chakula kukaa sana tumboni
✓ Wenye tatizo la kupungua kiwango cha acid tumboni
✓ Wenye magonjwa ya mfumo wa kinga ya mwili yaani Autoimmune diseases
✓ Wenye size ndogo ya tumbo
n.k
DALILI ZA TATIZO HILI LA gastric trichobezoar NI PAMOJA NA;
- Mtu kupata kichefuchefu pamoja na kutapika
- Kuhisi kushiba haraka baada ya kula chakula kidogo sana
- Uzito wa mwili kupungua kwa kasi sana
- Kukosa hamu ya kula chakula
- Kupata maumivu ya tumbo mara kwa mara
- Na pia mtu huweza kuona baadhi ya nywele kwenye kinyesi chake
n.k
MATIBABU YA UGONJWA HUU WA gastric trichobezoar
- Tatizo hili huweza kutibiwa kwa njia mbali mbali kama vile; Kutumia dawa za kudissolve hizo nywele ili ziweze kupita zenyewe au kutumia Njia ya upasuaji .
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!