Ticker

6/recent/ticker-posts

UGONJWA WA PITYRIASIS ROSEA(chanzo,dalili na tiba)



 pityriasis rosea

• • • • •

UGONJWA WA PITYRIASIS ROSEA(chanzo,dalili na tiba)


Ugonjwa wa pityriasis rosea ni ugonjwa ambao huanza kama rashes au kovu dogo maeneo mbali mbali kama vile mgongoni,kifuani n.k kisha kuanza kusambaa maeneo mbali mbali ya mwili wako,


Tazama picha hapa Chini;




CHANZO CHA UGONJWA HUU WA PITYRIASIS ROSEA


- Mpaka sasa hakuna chanzo kamili kinachosababisha ugonjwa huu kugundulika, 


japo baadhi ya watafiti wa afya husema ugonjwa huu huhusishwa na maambukizi ya Virusi kama vile Herpes, ila hakuna ushahidi wa kutosha juu ya hili



DALILI ZA UGONJWA HUU WA PITYRIASIS ROSEA NI PAMOJA NA;


✓ Mtu kupata maumivu makali ya kichwa


✓ Mwili kuchoka kupita kawaida


✓ Mtu kupatwa na vidonda kooni yaani Sore throat


✓ Joto la mwili kuwa juu au mtu kuwa na homa


✓ Baada hizi dalili zote ndipo mgonjwa baadae huanza kutokewa na kovu kubwa katika maeneo mbali mbali mwilini kama vile;tumboni, kifuani au mgongoni na kovu hili kwa kitaalam hujulikana kama herald patch,


Baada ya Herald patch kutokea sehemu moja ya mwili huanza kusambaa maeneo mbali mbali ya mwili.


✓ Mgonjwa kuendelea kupatwa na hali ya miwasho kwenye ngozi yake


MATIBABU YA UGONJWA HUU WA PITYRIASIS ROSEA


- Ugonjwa huu hauhitaji matibabu kwani hupona wenyewe ndani ya wiki 4 mpaka 10,


japo kama mgonjwa hupata madhara zaidi kama kuwashwa sana n.k, akutane na wataalam wa afya ili kupatiwa matibabu zaidi.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

 



Post a Comment

0 Comments