Q FEVER
• • • • •
UGONJWA WA Q FEVER(chanzo,dalili,madhara na Tiba)
CHANZO
Ugonjwa wa Q fever ni ugonjwa ambao husababishwa na bacteria wanaojulikana kwa jina la Bacterium Coxiella Burnetii,
Bacteria hawa husambazwa kwenda kwa binadamu kupitia wanyama kama vile; Mbuzi,kondoo n.k
DALILI ZA UGONJWA WA Q FEVER NI PAMOJA NA;
✓ Joto la mwili kuwa juu sana Mfano; 41 °C
✓ Mgonjwa kupata tatizo la kuharisha
✓ Kupata kichefuchefu pamoja na kutapika
✓ Mgonjwa kukohoa mara kwa mara
✓ Mwili kutetemeka
✓ Mwili kuchoka kupita kawaida
✓ Mgonjwa kupata maumivu makali ya Kichwa
MADHARA YA UGONJWA WA Q FEVER
- Ugonjwa huu huweza kuharibu Mapafu,Ubongo,Ini pamoja na Moyo
- Ugonjwa huu huweza kusababisha kuvimba kwa kuta za ndani ya moyo yaani kwa kitaalam Endocarditis
- Ugonjwa huu huweza kusababisha shida kwenye mapafu kama vile; Pneumonia n.k
- Ugonjwa huu huweza kusababisha matatizo mbali mbali kwenye ujauzito kama vile;mimba kutoka zenyewe,mtoto kuzaliwa kabla ya wakati(premature), mtoto kuzaliwa na uzito mdogo,mtoto kuzaliwa mfu n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!