Ticker

6/recent/ticker-posts

ATHARI ZA DAWA ZA KULEVYIA



 DAWA ZA KULEVYIA

• • • • • •

ATHARI ZA DAWA ZA KULEVYIA


Madhara ya kutumia madawa ya kulevyia ni mengi sana ambapo huweza kumpata mtu moja kwa moja au jamii inayomzunguka pamoja na taifa kwa ujumla,


Hapa tunazungumzia madawa kama heroin, bangi,kokeini n.k


Kuna madhara ya muda mfupi na kuna madhara ya muda mrefu au yakudumu,


1. MADHARA YA MUDA MFUPI NI PAMOJA NA;


- Hamu ya chakula kupotea kabsa kwa baadhi ya waathiriwa wa madawa ya kulevyia


- Na kwa baadhi yao hamu ya chakula huongezeka na kula kupita kawaida


- Mtu kukosa usingizi kabsa


- Kupatwa na tatizo la mapigo ya moyo kwenda mbio mara kwa mara


- Kuwa na tatizo katika matamshi ya baadhi ya maneno wakati wa kuongea


- Mwili kutetemeka ikiwa ni pamoja na mdomo,mikono n.k


- Kuwa na mahusiano mabaya katika jamii,familia,ndoa kuvunjika n.k



2. MADHARA YA MUDA MREFU NI PAMOJA NA;


- Mwili kuwa dhoofu,kukosa nguvu na mtu kukonda kupita kawaida


- Kupatwa na maambukizi ya magonjwa mbali mbali ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa UKIMWI


- kuwa katika hatari ya kupatwa na kansa au saratani mbali mbali kama vile; saratani ya ngozi, Koo,mapafu n.k


- Kupatwa na magonjwa mbali mbali ya moyo ikiwa ni pamoja na moyo kuwa mkubwa,mishipa ya damu ndani ya moyo kuziba n.k


- Kupatwa na tatizo la Figo kufeli au kushindwa kufanya kazi


- Kupatwa na tatizo la mapafu ikiwa ni pamoja na mapafu kujaa maji, vifuko vya hewa yaani Alveoli ndani ya mapafu kutoboka n.k


- Kupatwa na magonjwa ya ubongo, matatizo ya akili,mtu kuchanganyikiwa n.k


- Kufanya maamuzi mabaya kama vile kujiua au kuua mtu mwingine


- Kupatwa na magonjwa mbali mbali ya Ini,ikiwa ni pamoja na Ini kuvimba, Ini kushindwa kufanya kazi n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments