Ticker

6/recent/ticker-posts

CHANZO CHA TATIZO LA CHUCHU KUWASHA



 CHUCHU

• • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA CHUCHU KUWASHA


Baadhi ya wanawake hupatwa na tatizo hili la chuchu kuwasha sana,je chanzo cha tatizo hili ni nini?


CHANZO CHA TATIZO LA CHUCHU KUWASHA NI PAMOJA NA;


- kuwa na tatizo ambalo huhusisha ngozi kuvimba maarufu kama Atopic Dermatitis


- Kuwa na shida ya ngozi kukauka kupita kiasi hasa ngozi ya matiti au ngozi kuzunguka chuchu


- Hali ya mwanamke kuwa mjamzito huongeza sana uwezekano wa tatizo la chuchu kuwasha


- Ngozi ya chuchu au titi kuvutika kupita kawaida yaani Stretching


- Maambukizi ya magonjwa kwenye tisu za ziwa au kwa kitaalam Mastitis huweza kusababisha tatizo la chuchu kuwasha


- Na mara chache kwa wanawake wenye tatizo la Kansa ya matiti au Breast cancer huweza kupatwa na hali hii.


TATIZO HILI LA CHUCHU KUWASHA HUWEZA KUAMBATANA NA;


✓ ngozi ya titi kuwa nyekundu


✓ kuwa na vipele kwenye titi au chuchu


✓ Kuwa na vidonda kwenye titi au chuchu


✓ Chuchu kutoa damu au usaha


✓ maumivu makali ya titi


✓ Titi kuwa gumu kupita kawaida


✓ titi kuvimba na kuongezeka ukubwa

N.k



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments