Ticker

6/recent/ticker-posts

MAAMBUKIZI HATARI YA BACTERIA LISTERIA(listeria infection)



 LISTERIA INFECTION

• • • • •

MAAMBUKIZI HATARI YA BACTERIA LISTERIA(listeria infection)


Listeria infection ni maambukizi ya bacteria wanaojulikana kwa jina la LISTERIA, haya ni miongoni mwa maambukizi hatari ya Bacteria ambayo huweza kusababisha madhara makubwa kwa;


• Wanawake wajawazito


• Watu wenye umri wa zaidi ya miaka 65


• Na Wenye kinga ndogo ya mwili


CHANZO CHA BACTERIA HAWA WA LISTERIA


Bacteria hawa hupatikana kwenye Udongo, Maji au kwenye kinyesi cha wanyama ambapo mtu huweza kuwapata kwa njia mbali mbali kama vile;


- Kunywa maji machafu


- Kula mboga za majani ambazo zina bacteria hawa


- Kula nyama ambayo ina Bacteria hawa


- Kunywa maziwa ambayo yana Bacteria hawa


- Au kula chakula chochote ambacho kina bacteria hawa


DALILI ZA MAAMBUKIZI YA BACTERIA wa Listeria ni Pamoja na;


• Mtu kuwa na homa


• Mwili kuanza kutetemeka


• Kupata maumivu makali ya misuli


• Kupata kichefuchefu na kutapika


• Kuharisha


• Maumivu makali ya kichwa


• Shingo kukakamaa


• Kupata shida ya kupumua


• Kuwa na dalili za kama kuchanganyikiwa

N.k


MADHARA YA BACTERIA LISTERIA KWA WAJAWAZITO


✓ Ujauzito au mimba kutoka zenyewe


✓ Kuzaa mtoto mfu


✓ Kuzaa mtoto kabla ya wakati


✓ Kuzaa mtoto mwenye shida ya uzito mdogo sana


KUMBUKA; maambukizi haya kwa asilimia kubwa huweza kupona yenyewe,ila ni muhimu sana mtu kupata vipimo na kuongea na wataalam wa afya,ikiwezakana apewe antibiotics kwa ajili ya Infection hii,ili kuepuka madhara yake.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments