Ticker

6/recent/ticker-posts

MADHARA YA KUNYWA VINYWAJI VYENYE SUKARI NYINGI KILA SIKU



 SUKARI

• • • • • •

MADHARA YA KUNYWA VINYWAJI VYENYE SUKARI NYINGI KILA SIKU


Matumizi ya vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha sukari kila siku,huweza kusababisha madhara makubwa kwenye miili yetu.


MIONGONI MWA MADHARA YA KUNYWA VINYWAJI VYENYE KIWANGO KIKUBWA CHA SUKARI KILA SIKU NI PAMOJA NA;


- Kuwa katika hatari ya kupatwa na Ugonjwa Wa kisukari hasa aina ya kisukari ambayo hujulikana kama DIABETES TYPE 2


- Kuwa katika hatari ya kupatwa na tatizo la Gout


- Kuwa katika hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo


- Kuwa katika hatari ya kupatwa na tatizo la uzito na unene kupita kiasi yaani Obesity


- Kuwa katika hatari ya kupatwa na matatizo ya meno kama vile,meno kuuma kutokana na kuoza au kutobolewa na bacteria


- Kuwa katika hatari ya kupatwa na matatizo ya Figo ikiwa ni pamoja na tatizo la mawe kwenye Figo yaani Kidney stones


- kuwa katika hatari ya kupata matatizo kwenye mfumo wa umeng'enyaji chakula pamoja na uchakataji wake ndani ya seli, tatizo ambalo hujulikana kama Metabolic Syndrome.


Epuka kunywa vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha sukari kila siku kwani sio salama kwa afya yako.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments