Ticker

6/recent/ticker-posts

MAMBO YA KUZINGATIA ILI USIPATE VIDONDA KWA MGONJWA WA KISUKARI



  AFYA TIPS

• • • • • •

MAMBO YA KUZINGATIA ILI USIPATE VIDONDA KWA MGONJWA WA KISUKARI


Una kisukari au mtu wako wa karibu ana tatizo hilo? Watu wanaoishi na tatizo la kisukari huwalazimu kuwa makini sana ili wasipate vidonda vya aina yoyote ile, kwani huweza kuwa vigumu vidonda hivo kupona,


Haya hapa ni baadhi ya mambo yakuzingatia ili usipate vidonda vya aina yoyote hasa kwa wewe ambaye ni mgonjwa wa kisukari



1. Epuka kutembea bila viatu, yaani kutembea peku, kwa maana unaweza kujikata na kitu chenye ncha kali kama sindano, chumba, miiba n.k


2. Epuka kutumia vitu vyenye ncha kali kukatia kucha kwa mfano usitumie wembe au mkasi kukata kucha ili kuepuka kujikata na kupata kidonda, pendelea sana kutumia nail cutter.


3. Epuka kuvaa viatu na soksi za kubana, na pia hakikisha miguu yako ni mikavu kila muda, kwa hiyo basi utokapo kuoga ama kunawa miguu, hakikisha unaikausha vizuri hasa katikati ya vidole, kwa sababu kama ukiacha unyevunyevu ni rahisi kutengeneza lengelenge na pia endapo utapata lengelenge usitumbue na liache likauke lenyewe.


Kwa wanawake, epuka kuvaa viatu virefu kwa sababu vinazuia damu kufanya mvunguko wake wa kawaida (blood circulation)


#afyabongo #afyaclass


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments