Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwanamke kabeba mimba wakati bado mtoto ananyonya je anaruhusiwa Kumnyonyesha?



 UZAZI

• • • • • •

Mwanamke kabeba mimba wakati bado mtoto ananyonya je anaruhusiwa Kumnyonyesha?


Hili ni swali ambalo nimeulizwa na watu wengi sana naomba leo nitoe ufafanuzi katika makala hii,


MAJIBU;


Ndyo unaruhusiwa kumnyonyesha mtoto hata kama umebeba mimba nyingine wakati bado mtoto ananyonya, ila fahamu mambo haya;


✓ Mwili wako utaendelea kuzalisha maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto anayenyonya ujauzito ukiwa katika hatua za mwanzoni, ila kadri ujauzito unavyokuwa ndipo na uzalishaji wa maziwa hupungua kwa kiwango kikubwa, hasa ujauzito ukiwa na umri wa miezi 5 na kuendelea


✓ Kadri ujauzito unavyokuwa ndipo na Content za maziwa zinabadilika kama vile COLESTRUM hali ambayo hupelekea ladha ya maziwa kubadilika kabsa,


Hali hii huweza kusababisha mtoto asipate maziwa ya kutosha, kupata maziwa mepesi,kutokushiba N.k,


Hivi vyote huanza kuathiri ukuaji wa mtoto wako na kumfanya mtoto kuwa dhaifu, mwenye kuumwa umwa n.k


Hivo lazima uongee na wataalam wa afya ili wakushauri cha kufanya ikiwa ni pamoja na Lishe sahihi kwa mtoto huyo


✓ Mtoto ataendelea kukuwa tumboni kama kawaida na kupata  virutubisho vyote muhimu kutoka kwa mama, kama mama anazingatia hatua za ulaji bora kwa mama mjamzito


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments