Ticker

6/recent/ticker-posts

UGONJWA WA ROSEOLA,Chanzo chake,Dalili na Tiba(Watoto)



  ROSEOLA

• • • • • •

UGONJWA WA ROSEOLA,Chanzo chake,Dalili na Tiba(Watoto)


Ugonjwa wa Roseola ni ugonjwa ambao unashambulia sana Watoto wadogo wenye umri wa Miaka 2, Wanaoingia KINDERGARTEN na mara chache sana Watu Wazima


DALILI ZA UGONJWA WA ROSEOLA NI PAMOJA NA;


- Mtoto huanza kupata Homa ya gafla ambapo mara nyingi JOTO lake la mwili linakuwa zaidi ya 39.4 °C


- Ikifwatiwa na kuwa na Rashes au vipele kwenye mwili wa Mtoto


- Kuvimba kwa Tezi za shingoni


- Mtoto kuanza kukohoa


- Kuwa na mafua au tatizo la Runny Nose


- Mtoto kuanza kuharisha


- Kukosa kabsa hamu ya kula chakula


- Mtoto Kuvimba macho

N.k


• Soma: Madhara ya Maziwa ya Kopo Kwa WATOTO wadogo


CHANZO CHA UGONJWA WA ROSEOLA


• Ugonjwa huu wa Roseola husababishwa na Aina Mbili za Virusi jamii ya HERPES VIRUS ambazo ni Human Herpes Virus 6 na Human Herpes Virus 7


Virusi hawa huweza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa Njia mbali mbali kama vile; ya mate,makamasi N.k


MATIBABU YA UGONJWA WA ROSEOLA


✓ Wagonjwa wengi hupona kabsa wiki moja baada ya kuwa na Homa Kali,


Dawa mbali mbali hutumika kama vile; Ibuprofen, Acetaminophen


Na Dawa jamii ya Antiviral Drugs kama vile GANCICLOVIR n.k


• Soma: Madhara ya Kutumia PODA kwa watoto


• Soma: Ugonjwa wa Tetekuwanga,chanzo na Tiba


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments