Ticker

6/recent/ticker-posts

Ally Dangote wa Arusha ambaye amechoma Watu 15 visu amefariki dunia



Kijana mmoja wa Jijini Arusha maarufu kwa jina la Ally Dangote ambaye kwenye siku za karibuni amekuwa akisakwa hadi picha zake kubandikwa kwenye mitaa mbalimbali kutokana na tuhuma za kuchoma Watu 15 visu, kuua Watatu huku akiwa anavalia hijabu ili kujificha, amefariki dunia leo baada ya kudaiwa kujirusha kutoka kwenye gari la Polisi wakati akiwapeleka Polisi kwenda kuwafichua Wahalifu wenzake.

Mamia ya Watu walifurika leo nje ya chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mount Meru Arusha wakitaka kushuhudia kama ni kweli Kijana huyo amefariki kwani amekua tishio kwa Wakazi wengi hasa kutokana na mfululizo wa matukio yake ya kutisha ikiwemo kuwabaka Wanawake.

“Sijaamini kama amekufa ndio maana nimeshikilia jiwe tunaweza kufanya mzaha ukakuta tu kazimia….. nimejihadhari na jiwe” amenukuliwa akiongea Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kama Mama Chuda ( picha ya pili ).

Via #MillardAyoUPDATES



Post a Comment

0 Comments