Ticker

6/recent/ticker-posts

Hakuna Mtanzania Anayeteswa Uarabuni



Balozi Abdallah Kilima ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amekanusha uvumi ambao umekuwa ukienezwa kuwa Watanzania wengi wanaofanya kazi katika nchi za Mashariki ya Kati wanateswa.

Akizungumzia manufaa yanayotokana na mkataba uliosainiwa kati ya Tanzania na Saudi Arabia ambao utawawezesha Watanzania kupata ajira katika sekta mbalimbali amesema, asilimia 92 ya wanaofanya kazi kwenye nchi hizo wananufaika, na asilimia nane iliyobaki wanaweza kuwa wanapitia changamoto mbalimbali kutokana na kutofuata taratibu.

Balozi Kilima amesisitiza kuwa nchi nyingi za Mashariki ya Kati zinategemea nguvu kazi kutoka nje, hivyo ni wakati sasa kwa Tanzania kuchangamkia fursa hiyo, huku akiongeza kuwa zipo nchi nyingjme tatu ambazo zimeomba kusaini mkataba kama huo na Tanzania ili kupata nguvu kazi.

Ameongeza kuwa Saudia Arabia inatarajiwa kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2034, na inaweka mikakati ya kuandaa maonesho ya kibiashara (Expo) mwaka 2030, hivyo ni wakati mwafaka kusainiwa kwa mkataba huo ambao utatoa ajira kwa maelfu ya Watanzania.



Post a Comment

0 Comments