Ticker

6/recent/ticker-posts

Idadi ya Wanaume wanaopima DNA yaongezeka Nchini Tanzania



Mkemia Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dr. Fidelis Mafumiko amesema idadi ya Wanaume wanaojitokeza kupima DNA ( kuhakiki uhalali wa Watoto wao ) imeongezeka kwa sasa Nchini Tanzania tofauti na miaka miwili hadi mitatu iliyopita.

Kwenye mahojiano mafupi na @dw_kiswahili Dr. Fidelis amenukuliwa akisema “naweza kusema elimu ile ya kujua kwamba kumbe kuna teknolojia inaweza kusaidia utambuzi wa Watoto, idadi ya Watu wanaojitokeza imeongezeka kidogo ukilinganisha na miaka miwili mitatu nyumba lakini hii yote imetokana na elimu ya vina saba kwa sababu kazi mojawapo tunayofanya ni kuwaelimisha”



Post a Comment

0 Comments