Ticker

6/recent/ticker-posts

Jipu kwenye uume, chanzo chake na Tiba yake



Jipu kwenye uume, chanzo chake na Tiba yake

Baadhi ya watu hupatwa na tatizo la kuwa na majipu au jipu kwenye Uume, je chanzo chake ni nini?

Jipu kwenye uume huweza kusababishwa na sababu mbali mbali ikiwemo;

  • maambukizi ya bacteria,
  • uchafu(poor hygiene),
  • Msuguano
  • au nywele zinazoota kwa ndani(ingrown hairs).

Soma Zaidi hapa kwenye makala hii kuhusu chanzo cha Jipu kwenye uume, na matibabu yake;

Chanzo cha Jipu kwenye uume

Majipu kwenye Uume huweza kutokana na Sababu mbali mbali ikiwemo;

– Maambukizi ya Bacteria, Hii ndyo sababu kubwa inayopelekea mtu kuwa na jipu au majipu kwenye Uume,

Kwa asilimia kubwa mtu huweza kuwa na jipu kwenye uume baada ya kushambuliwa na aina flani ya bacteria, na mara nyingi aina ya Staphylococcus aureus ndyo chanzo kikubwa.

Bacteria hawa huweza kupita kwenye ngozi baada ya kujikata hata kidogo, kupitia kwenye kidonda au kwenye shina na tundu la nywele sehemu za siri, na matokeo yake wakasababisha majipu au jipu.

– Uchafu(Poor Hygiene): kutokufanya usafi vizuri hasa maeneo ya sehemu za siri huweza kutengeneza mazingira mazuri kwa bacteria kuzaliana na kusababisha majipu.

– Tatizo la Genital Herpes: ambapo huhusisha maambukizi ya virus kwa kitaalam herpes simplex virus,

Maambukizi haya ya Virusi huweza kusababisha vidonda vyenye maumivu makali, malengelenge sehemu za siri, vipele, majipu n.k

– Ugonjwa wa kaswende: kaswende ni miongoni mwa magonjwa ya Zinaa ambayo huweza kupelekea mtu kuwa na vidonda, uvimbe au majipu kwenye uume,

Vidonda kwenye uume hutokea wakati ugonjwa wa kaswende ukiwa katika hatua ya pili. Kaswende ni maambukizi hatari na ni lazima kutibiwa na antibiotics.

– Tatizo la Molluscum Contagiosum: tatizo hili huhusisha maambukizi ya Virusi kwenye ngozi,

– Tatizo la Scabies: haya ni maambikizi ya parasite, uvamizi wa vimelea unaosababishwa na mite Sarcoptes scabiei,

Tatizo hili linaweza kusababisha kuwashwa, matuta mekundu yaliyoinuliwa na mashimo madogo kwenye ngozi. Scabies inahitaji matibabu.

– Saratani ya Uume(Penile Cancer): Saratani kwenye uume huweza kupelekea vidonda,uvimbe,vitu kama majipu kwenye uume.

– Uchafu(Poor Hygiene): kutokufanya usafi vizuri hasa maeneo ya sehemu za siri huweza kutengeneza mazingira mazuri kwa bacteria kuzaliana na kusababisha majipu.

– Msuguano mkali(Friction and Irritation), Msuguano kutokana na kuvaa nguo ya kubana sana, msuguano wakati wa tendo la ndoa, au hata wakati wa kunyoa nywele sehemu za siri huweza kupekelea hali ya ngozi ya uume kuwashwa,kuvimba,kuchanika n.k

Matokeo yake uume unakuwa kwenye  hatari zaidi ya kupata maambukizi ya bacteria kama vile Staphylococcus aureus ambao huweza kupelekea kutokea kwa majipu

– Magonjwa kama Peyronie’s Disease: Peyronie’s disease ni tatizo ambalo huhusisha kukua kwa fibrous plaques kwenye ngozi ya uume au shimoni,

– Pamoja na Matatizo mengine kama vile Lichen Planus n.k

Sababu hizi, kwa moja moja au kwa pamoja, zinaweza kusababisha kutokea kwa majipu kwenye uume, ambayo yanaweza kusababisha maumivu makali.

Ikiwa una jipu kwenye uume wako, hakikisha unatafuta matibabu sahihi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments