Ticker

6/recent/ticker-posts

kifo Cha mjamzito Mariam Zahoro kilitokana na uzembe sio kukosa fedha za matibabu kiasi cha Tsh. 150,000



Tume iliyoundwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuchunguza kifo Cha mjamzito Mariam Zahoro imesema kifo hicho kilitokana na uzembe wa Wataalamu wa Afya na sio kutokana na kukosa fedha za matibabu kiasi cha Tsh. 150,000.

Kifo cha Mariam Zahoro kilitokea November 11,2023 katika Kituo cha Afya cha Kabuku Mkoani Tanga baada ya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida na kuhitaji kufanyiwa upasuaji na kuchelewa Kwa huduma ya dharura ya upasuaji.

Akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kabuku Waziri Ummy amesema tayari Baraza la Madaktari pamoja na Wauguzi na Wakunga linaendelea na utaratibu wa kuchukua hatua za kinidhamu kwa Wataalamu wawili wa afya katika kituo hicho.

“Tutahakikisha baada ya hili hakuna kifo kinachotokana na uzembe kinatokea hapa nchini kwani tumejipanga kuchukua hatua kali ili iwe fundisho kwa Watumishi wa Afya wazembe”

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Dkt. Ali Said amesema chanzo cha kifo ni kutokana na uzembe wa Wataalamu hao kushindwa kuchukua hatua za haraka Ili hali mgonjwa akiwa katika hali ya hatari “Mwanamke huyo alichelewa kupatiwa huduma ya upasuaji kutokana na kukosekana kwa Mtaalamu wa dawa ya usingizi ambaye hakuwa anapatikana huku Daktari wa upasuaji akishindwa kutoa maamuzi ya rufaa kwa wakati kwenda kwenye Hospitali ya Wilaya”



Post a Comment

0 Comments