Ticker

6/recent/ticker-posts

KONGO:kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Disemba 20 zimeanza



Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Disemba 20 zimeanza kuanzia jana Jumapili. Rais Tshisekedi anayewania muhula wa pili alianza kampeni katika mji wa Kinshasa.

Kampeini za uchaguzi nchini Kongo zinaendelea hii leo ambapo mgombea mkuu wa Upinzani Moise Katumbi anatarajiwa kuanzisha kampeini yake katika mji wa Kisiangani,mkoani Tshopo leo, kuwashawishi wapiga kura.

Rais anayetetea nafasi yake Felix Tshisekedi ni miongoni mwa waliozindua rasmi kampeini zao    hapo jana Jumapili.

Katika Uwanja wa mashujaa mjini Kinshasa  rais Félix Tshisekedi anayegombea tena urais kwa muhula wa pili, alianzisha kampeni yake ya uchaguzi.

Alisifu mafanikio yake akisisitiza elimu bila malipo na kueleza kwamba washirika wake wa zamani wa FCC, yaani muungano wa kisiasa wa raïs wa zamani Joseph Kabila walikuwa wakitilia mashaka.

Soma pia:Kampeni za uchaguzi mkuu kuanza rasmi tarehe 20.11.2023 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

“Nilipoanzisha elimu bila malipo, ndugu zetu wa FCC waliniambia kuwa sitafanikiwa,” aliwaambia wapiga kura rais Tshisekedi.

Aliongeza kuwa kutokana na mshikamano ambao unashuhudiwa nchini humo aliona mwangaza wa kufanikiwa kwa sera hiyo ambayo ilikuwa ikipigwa vita na baadhi ya wanasiasa ikiwemo wapinzani.

Alisisitiza umuhimu wa kujitosa katika sera hiyo kwa kurumia rasilimali chache zilizopo.

“Ni lazima kuanza na baadae ndipo tutajua kama tutafanikiwa au la.”



Post a Comment

0 Comments