Ticker

6/recent/ticker-posts

Loveness Tarimo aeleza changamoto anazokutana nazo kutokana na mwonekano wake wa Kiume



Loveness Tarimo ni mwanamke mtunisha misuli anayeshikilia nafasi ya Miss Fitness Tanzania na Miss Fitness East Afrika.

Global TV imefanya naye Exclusive Interview ambapo amefunguka changamoto mbalimbali anazokutana nazo kutokana na mwonekano wake na kusisitiza kwamba yeye ni mwanamke na ana jinsia ya kike.

Amesema miongoni mwa changamoto hizo, ni kwenye matumizi ya vyoo vya umma ambapo huwa ni lazima aongozane na mtu mwingine anapoingia kwenye vyoo vya wanawake kwa sababu watu hudhani kama ni mwanaume anayeingiakwenye vyoo vya wanawake.

Source: Globalpublishers



Post a Comment

0 Comments