Ticker

6/recent/ticker-posts

Magonjwa ambayo yana dalili zinazofanana na dalili za HIV



Fahamu kwamba baadhi ya dalili za Ukimwi huweza kufanana na dalili za magonjwa mengine,

mfano; dalili kama homa,uchovu kupita kiasi, kupata vipele kwenye ngozi n.k

Hivo basi, si kila mtu mwenye dalili kama hizi basi ana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU), fanya vipimo kwanza.

Baadhi ya watu wamekutana na changamoto ya kuanza kupata dalili kama hizi ambazo huendana kabsa na dalili za Ukimwi baada ya kushiri tendo na watu ambao wanadhani hawapo salama,

Hali ambayo inapelekea hofu kubwa sana kwao, lakini pia wakija kupima hawaoni Ugonjwa wowote, je hii ikoje?

Fahamu hapa mambo mawili ya Msingi kama upo kwenye hali kama Hii;

(1) Ili kipimo cha HIV kisome na kutoa majibu kama umeathirika lazima mwili wako uwe umeshatengeneza HIV-antibodies,

Hizi antibodies hazitengenezwi siku hiyo hyo baada ya kuambukizwa, huchukua muda kidogo.

(2) Unaweza kuwa na dalili zote ambazo zinaweza kukufanya ufikirie kwamba umeambukizwa, kumbe una magonjwa mengine yenye dalili zinazofanana na za Ukimwi.

Magonjwa ambayo yana dalili zinazofanana na dalili za HIV

Dalili za VVU ni tofauti katika hatua za mwanzo na za mwisho za maambukizi, Dalili za kwanza huonekana ndani ya wiki 2 hadi 4 baada ya kuambukizwa, na zinaweza kujumuisha:

  • Kupata homa za mara kwa mara
  • Uchovu wa mwili kupita kiasi
  • Kupata maumivu ya misuli
  • Kupata vipele kwenye ngozi
  • Kuhisi hali ya vidonda kooni(Sore throat)
  • Kuvimba kwa tezi(Swollen glands)
  • Kuharisha
  • Kupata vidonda Mdomoni n.k

Hivo basi, dalili za mwanzoni za maambukizi ya virusi vya Ukimwi(VVU) ikiwemo hizi; Homa, maumivu ya misuli, uchovu wa mwili kupita kiasi, Mafua mara kwa mara pamoja na vidonda mdomoni na kooni huweza kufanana kabsa na dalili za magonjwa mengine ikiwemo;

(1) Ugonjwa wa homa ya Mafua, maambukizi ya Virusi vya Influenza(Flu)

(2) Tatizo la Mononucleosis (mono)

(3) Tatizo la Strep throat

(4) COVID-19

(5) Maambukizi ya Virusi kama vile Epstein-Barr virus

(6) Maambukizi ya virusi wanaosababisha ugonjwa wa ini kama vile Viral hepatitis n.k

(7) Baadhi ya Magonjwa ya Zinaa

(8) Lakini pia mgonjwa anaweza kuwa na Upele ambao unafanana kabsa na ule ikiwa mgonjwa ana maambukizi ya HIV hatua ya mwanzo(early stage of HIV infection),

Upele huu unaweza kuashiria magonjwa Au matatizo mengine ya kiafya mbali na HIV, Kama vile;

  • Kuwa na shida ya Mzio(Allergic reactions)
  • Maambukizi ya Herpes
  • Kuwa na hofu,Msongo wa mawazo au Stress
  • Upele kwenye ngozi kutokana na Kemikali kwenye baadhi ya bidhaa kama shampoo na Sabuni
  • Maambukizi ya virusi kama vile Roseola(viral infection)

(9) Kuharisha kunaweza kutokana na maambukizi ya virusi tumboni, kula viambato vya sumu(food poisoning),au magonjwa mengine mengi huweza kusababisha shida hii

(10) Vidonda Mdomoni(Mouth Sore) huweza kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo

  • kuungua,
  • kuumia kwa namna yoyote,
  • kupata maambukizi ya oral herpes,
  • tatizo la mzio(allergy),
  • Au upungufu wa baadhi ya vitamini(vitamin deficiency).n.k

(11) Kuwa na Homa, hiki ni kiashiria kwamba kinga yako ya mwili inajaribu kupambana na maambukizi ya ugonjwa wowote,

Hivo magonjwa au maambukizi mbali mbali yanaweza kupelekea wewe kuwa na Homa ikiwemo;

– Maambukizi ya Virusi na bacteria(Viral and bacterial infections)

– Tatizo la Rheumatoid arthritis  pamoja na inflammatory diseases zingine.

– Saratani

– Pia hata baadhi ya dawa,mfano baadhi ya antibiotics pamoja na anti-seizure medications.

(12) Kutoa sana jasho wakati wa Usiku,

Hii inaweza kuwa dalili ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) hasa maambukizi yakiwa kwenye hatua za mwisho(Late-stage HIV or AIDS), ingawa yapo magonjwa au hali zingine za kiafya ambazo huweza kusababisha tatizo hili ikiwemo;

  • Mwanamke kuingia kipindi cha ukomo wa hedhi(Menopause)
  • Shida ya Overactive thyroid gland
  • Tatizo la kiharusi au Stroke
  • Kuwa na Ugonjwa wa TB(Tuberculosis) pamoja na maambukizi mengine
  • Kuwa na Saratani kama vile; Saratani ya damu(leukemia), non-Hodgkin’s lymphoma n.k

Rejea za mada;



Post a Comment

0 Comments