Ticker

6/recent/ticker-posts

Mifugo 303 yakamatwa ikisafirishwa kwenda nje ya nchi



Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia doria ya pamoja wamekata watuhumiwa wawili wakiwa na mifugo 303 kwa madai ya kuisafirisha kwenda nje ya nchi kwa njia za magendo bila vibali.

Akitoa taarifa hiyo maeneo ya mnada wa Longido, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Simon Pasua leo Jumapili Novemba 19, 2023 amebainisha kuwa mifugo hiyo pamoja na watuhumiwa hao wamekamatwa eneo la Buguruni C, Wilaya ya Longido mkoani Arusha.

Kamanda Pasua amesema bado wanaendelea na upelelezi, na pindi utakapokamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.



Post a Comment

0 Comments