Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwanamitandao afariki baada ya kufanya upasuaji wa kurekebisha shape



Mwanamitandao wa huko Brazil #LuanaAndrede (29) amefariki dunia muda mchache baada ya kufanyiwa Surgery, Tukio hilo lilitokea katika Hospitali ya São Luiz huko São Paulo, ambapo Andrade aliandamana na familia yake kwa ajili ya upasuaji wa urembo.

Kulingana na jarida la People, wakati wa upasuaji huo, uliochukua takriban masaa mawili na nusu, Andrade alipata tukio la kupumua kwa ghafla, na kusababisha mshtuko wa moyo na mishipa kuziba kupitisha damu.

Hospitali ilitoa taarifa iliyosema, “Upasuaji ulikatizwa, na mgonjwa alifanyiwa vipimo vilivyoonyesha mvilio kwenye mishipa ya damu na kupelekwa ICU, ambako alipatiwa dawa na matibabu”.



Post a Comment

0 Comments