Ticker

6/recent/ticker-posts

Namsaidia Mke Wangu Kufua, Kudeki pamoja na Kupika Bila kuona Aibu-Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amewasihi Wanaume kuwasaidia Wake zao kazi za nyumbani kama vile kupika na kufua bila kuona aibu na kuachana na tamaduni za kuamini kazi hizo wanafanya Wanawake pekee ambapo amesema yeye akiwa nyumbani Weekend huwa anafua nguo zake na za Mke na Watoto na kupika pia.

Chalamila amesema hayo wakati wa sehemu ya pili ya mahojiano maalum aliyofanya na Mwandishi wa @AyoTV_, Bakari Chijumba ambapo ameongelea mambo mbalimbali ikiwemo maisha yake anapokuwa nyumbani na Familia “Jumamosi na Jumapili huwa ninaingia zamu ya kupika, naingia pia zamu ya kufua nguo za Mke wangu na za kwangu mwenyewe, huwa sioni aibu kupika, kudeki, kufua nguo n.k”

“Kuhusu Wanaume wasiofua na kupika nyumbani ni utamaduni ambao tumeukuta kwamba Baba ni Baba kweli na kwa maana hiyo Mwanamke ndio anafanya wewe haufanyi lakini leo tumeona Wanawake wamekua kiuchumi, kuna nyumba Mwanamke ndio Baba wa nyumba kuna maeneo Wanaume wamepoteza muelekeo na hawatambui majukumu yao, kumuoa Mwanamke hakumaanishi Mwanamke anakabidhi uhuru na madaraka kwako, wote mnakuwa na majukumu kulingana na muktadha, tuache kufikiri kwamba kupika, kufua sio haki ya Mwanaume hapana, ukifanya hivyo maana yake hata ukifiwa unatakiwa nawe ufe”

“Mimi napenda kusikiliza Injili lakini Watoto wanapenda sana miziki ya Bongofleva hii ya akina Diamond, Alikiba, Harmonize, Zuchu hata juzi mliona kule Watoto wanacheza Honey ya Zuchu na nilishukuru sana Bunge maana sidhani kama Watoto walifundishwa na yule Mwalimu, pale nyumbani nina kinanda na naimba nina album fulani itatoka muda wowote, nataka nichukue nafasi ya marehemu Komba, nataka nipige muziki mzuri nimuoneshe Katibu Mkuu wa CCM na Mwenezi Ndugu yetu Makonda waangalie ilivyokaa kama naweza kuwa mbadala wa TOT na najiandaa sana kipindi cha uchaguzi, Watanzania waniunge mkono”



Post a Comment

0 Comments