Ticker

6/recent/ticker-posts

Njia ya Jangwani katika Barabara ya Dar es Salaam - Morogoro imefungwa muda huu



Njia ya Jangwani katika Barabara ya Dar es Salaam – Morogoro imefungwa muda huu kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika Jiji la Dar es Salaam.

Wasafiri wanashauriwa kutumia usafiri mbadala ikiwemo daladala mpaka Morocco kwa wale wanaotokea Posta kwenda Kimara. Wakifika Morocco wanaweza kuendelea na usafiri wa DART mpaka Kimara na sehemu nyingine za Jiji

Kwa wasafiri wanaoelekea Posta kutoka Kimara, wameshauriwa kuchukua mabasi ya DART mpaka Morocco ambapo wanaweza kuchukua usafiri mbadala ikiwemo daladala mpaka Posta, Kariakooo na sehemu nyingine za Jiji.

Una maoni usisite kutuandikia.



Post a Comment

0 Comments