Ticker

6/recent/ticker-posts

Simu bila button ilivumbuliwa kwa staili hii



Mwanzoni kwa mwaka 2005, mwanzilishi wa kampuni ya Apple, Steve Jobs aliwapa wafanyakazi wake mtihani mgumu.

Aliwapa siku 15 za kuja na idea kali ya nini cha kutengeneza la sivyo itabidi afanye maamuzi magumu. Na kweli baada ya wiki 2 moja ya idea ilikuwa kutengeneza kifaa ambacho hakitakuwa na button lakini kiendeshwe kwa kuguswa.

Baada ya muda mrefu wa kufanyia kazi idea hii, swali likaja kama haina button tunawezaje kuzuia mtu kubonyeza vitu kwa bahati mbaya? Na pia, mtu ana unlock vipi? (Kabla ya hapo ilikuwa unashikiria nyota, unakumbuka?)

Jibu lilipatikana kama utani. Mmoja ya wafanyakazi kwa jina la Freddy Anzures alikuwa anasafiri na ndege kutoka New York kwenda San Francisco.

Alipokuwa akienda chooni, akagundua namna milango wa chooni ubafunguliwa kwa urahisi sana kwa kuslide tu. Hapo ndio feature ya “Slide to Unlock” ilipozaliwa, kama unavyoona kwenye picha.

Ubunifu ni kuunganisha mawazo. Wakati mwingine, jibu la changamoto lako lipo nje kabisa ya fani yako.



Post a Comment

0 Comments