Ticker

6/recent/ticker-posts

UTPC:kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia



Katika kuendelea kuunga mkono Serikali Kupinga Vitendo vya kikatili Nchini ,Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania leo umezindua rasmi kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, ambapo imelenga kuwaunganisha waandishi wa habari nchini pamoja na wadau wengine kupaza sauti kwa pamoja kupinga vita vitendo hivyo.

Akizindua kampeni hiyo kwa niaba ya Rais wa UTPC, Deo Nsokolo, Mjumbe wa Bodi ya UTPC, Lilian Lucas amesema kuwa waandishi wa habari wanayo nafasi kubwa kupitia kalamu zao kuhakikisha vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto vinakomeshwa.

Amesema wanahabari wanadhamana kubwa katika kuhakikisha jamii inatambua madhara ya ukatili kwa jamii hivyo wanapaswa kutumia kalamu zao vizuri kupata sauti

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Keneth Simbaya amesema kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto ni miongoni mwa ukiukwaji mkubwa uliokithiri wa haki za binadamu na kuwataka wanahabari kushiriki vyema katika kuielimisha jamii hasa juu ya sera, sheria pamoja na miongozo ambayo itasaidia kuleta mabadiliko na kupunguza ama kuondoa kabisa ukatili.



Post a Comment

0 Comments