Ticker

6/recent/ticker-posts

Vitundu vya pua vyaziba baada ya kuficha mistari ya kuzeeka (picha)



Mwanamke mmoja ambaye aliamua kupata huduma ya face fillers ili kuficha mistari  inayoonyesha “kuzeeka” hasa wakati wa kutabasamu, kwa bahati mbaya huduma ilienda vibaya sana na kusababisha pua yake kutoka na kudondoka pamoja na vitundu vya pua kuziba(nostrils).

Krysta Carson, kutoka Seattle, Washington, anasema daktari wake alimdunga sindano “ya kutatanisha” kwenye mshipa mkubwa wa damu, ambayo ilisababisha mwili wake kufa ganzi wiki mbili baadaye.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 52 aliamua kupata dermal filler ili kuficha mistari ya kuzeeka kwenye ngozi ambayo ilikuwa inaonekana sana hasa wakati akitabasamu.

Krysta anasema alikuwa amedungwa kichungi kwenye mistari ya tabasamu kila mwaka tangu 2016 na alipenda matokeo, kabla ya kuziba kwa mishipa mnamo 2020,na kusababisha ngozi ndani ya mdomo wake, pua na karibu na pua yake ya kushoto kuwa necrotic na kuanguka.

Baadhi ya Picha za kutisha zilionyesha jinsi pua yake yote ilivyobadilika kuwa nyeusi na kuoza, kabla haijadondoka.

Mtumbuizaji huyo mtaalamu anasema “alipoteza tumaini la kuishi” baada ya hali ya mshtuko kuharibu kazi yake ya miaka 30, licha ya daktari wake kudai kuwa atakuwa sawa ndani ya wiki sita za tukio hilo.

Pia Krysta anasema kuwa anashukuru mumewe, Redd Gill mwenye umri wa miaka 42, maana alipata mtaalamu wa viungo bandia vya usoni baada ya kukesha akifanya utafiti.



Post a Comment

0 Comments