Ticker

6/recent/ticker-posts

Wanajeshi wa Israel tayari waingia hospital ya Gaza,Al Shifa



Jeshi la Israel limefanya operesheni dhidi ya Hamas iliyolenga moja kwa moja hospitali ya Al Shifa mjini Gaza. Jeshi hilo limetaka kujisalimisha kwa watu linaowaita magaidi.

Mtu aliyekuwa ndani ya hospitali ya Al-Shifa amemwambia mwandishi wa BBC Rushdi Abu Alouf kwamba a wanajeshi wa Israel wameanza kuivamia.

“Askari walirusha bomu la machozi ambalo lilisababisha watu kukosa hewa,” anasema Khader Al-Zaanoun.

“Niliona wanajeshi wakiingia katika idara maalumu ya upasuaji,” Khader aliniambia kabla ya mawasiliano naye kukatika, anasema Rushdi.

Hii ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa Isarel wameingia ndani ya hospitali ya Al-Shifa baada ya siku kadhaa za mashambulizi na mapigano makali huko Gaza.

Awali,msemaji wa idara ya afya Gaza Ashraf al Qidra aliwaomba viongozi wa Misri,Qatar na Umoja wa Mataifa kuingilia kati kuokoa maisha ya wagonjwa na wafanyakazi walioko ndani ya hospitali hiyo.

Al-Shifa ndiyo hospitali kubwa zaidi huko Gaza, na Israel na Marekani zinadai kuwa Hamas ina kambi yake kuu – ambayo Hamas inakanusha.

BBC haijafanikiwa kuthibitisha madai hayo ya Israel na Marekani.

Wafanyakazi wa misaada wanasema hali ndani ya Al-Shifa ni “mbaya” na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas inasema kuna maelfu ya watu wanaotumia eneo hilo kujikinga dhidi ya mashambulizi ya Israel.

Kituo hicho pia kinaishiwa na mafuta, maafisa wanasema, jambo ambalo limefanya kuwa vigumu kwa wafanyikazi kusaidia wagonjwa wanaohitaji huduma ya dharura – ikiwa ni pamoja na watoto wanaozaliwa kabla ya wakati ambao wametolewa kwenye vyumba maalum kutokana na kukatika kwa umeme, madaktari wanasema.

Hapo awali, daktari mmoja aliambia BBC kwamba takriban watu 200 wamezikwa katika kaburi la pamoja huko Al-Shifa, baada ya maiti zilizoharibika zilizorundikana katika hospitali hiyo.

Source:Bbc



Post a Comment

0 Comments