Ticker

6/recent/ticker-posts

Wanne wafariki dunia baada ya mtumbwi kupinduliwa na kiboko



Watu wanne wamefariki dunia, wawili wakiwa ni wa familia moja na wengine saba kujeruhiwa baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria wakitokea shambani kupinduliwa na kiboko katika Mto Rufiji, Kijiji cha Mloka mkoani Pwani.

Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Meja Edward Gowelle amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwaomba wananchi kutotumia mitumbwi ya asili na badala yake watumie boti za kisasa zilizowekwa rasmi kwa ajili ya kusafirishia watu na kuacha mara moja tabia ya kubeba watu wengi kwenye mitumbwi hiyo.



Post a Comment

0 Comments