Ticker

6/recent/ticker-posts

Watoto wenye changamoto za Via vya Uzazi na Jinsia Tata (Intersex) sasa kupata Utetezi nchini Tanzania



Muungano wa mashirika yanayotetea haki za watoto wenye changamoto za Via vya Uzazi na Jinsia Tata (Intersex) nchini Tanzania, leo wameelezea lengo lao na kuwatetea watoto wenye changamoto hizo ili waondokane na unyanyapaa na kufuta imani potofu kwa jamii inayoishi nao.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Tanzania Voice Of Humanity (TVOH), Baby John wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akizungumzia mpango wa kuwatetea watoto na watu watu wazima waliozaliwa na changamoto ya via vya uzazi au jinsi tata. Aliendelea kusema;

“Hali hii mtoto anazaliwa nayo akiwa na mapungufu yanayomfanya kushindwa kupata utambulisho kamili wa jinsi ya kike au kiume na inatokana na changamoto wakati wa uumbaji au utengenezaji viungo vya uzazi vya nje au vya ndani au vyote kwa pamoja”.

Amesema muungano wa hiari wa mashirika hayo yanayotetea haki za watoto wenye changamoto za Via vya Uzazi na Jinsi Tata nchini Tanzania wamesema inaaminika kuwa takribani watoto 30 kila mwezi wakiwa na changamoto za Via vya Uzazi au jinsi tata hapa nchini.

Ameeleza kuwa ni vyema umma uelewe tofauti ya Jinsia, Jinsi ambapo hiyo ni hali ya kuzaliwa nayo inayokutambulisha kuwa wewe ni mwanamke au mwanaume ambapo Jinsia ni hali inayojengwa na malezi na makuzi na Jamii inayokuzunguka inayofanya ubebe majukumu yanayohusiana na hali yako ya Ke na Me.

“Hali hii inaweza kugundulika wakati mtoto anapozaliwa, kipindi cha ukuaji,au wakati wa kubalehe kinachotokea ni kwamba wakati mtoto anapozaliwa via vya uzazi au viungo vya sehemu za siri huficha hali halisi, huchelewa au kushindwa kutoa tafsiri halisi ya kike ama kiume.

Kuhusu changamoto amesema kuwa mtoto mwenye hali ya jinsi tata au changamoto ya via vya uzazi anaweza kuonekana au asionekane wazi kwa macho ya kawaida.

Lakini pia anapoonekana anaweza asiwe na viashiria vya kimaumbile vinavyokubalika katika jamii na hii imechangia kwa kiasi kikubwa kujitokeza kwa tafsiri potofu kutokana na hali yake.

“Watoto wanaozaliwa na changamoto na hali hii wanakabiliwa na unyanyapaa mkubwa unaochangiwa na imani potofu na wanapokuwa watu wazima kutokana na changamoto ya muonekano au kushindwa kwao kushiriki za mgawanyo kijinsia katika jamii. Basi huwa katika hatari ya kuhusianishwa na tabia zisizo za kimaadili katika jamii.

“Hivyo nitoe wito kwa jamii na familia ni muhimu kupambanua na kuwa makini katika kutambua na kujifunza tofauti ya kuzaliwa na changamoto za Via vya uzazi na jinsi tata na ukiukwaji wa maadili na mila potofu, kama tunakubali changamoto wanazozaliwa nazo watoto za maumbile mengine katika mwili wa baadhi ya ndugu zetu.

Basi ni vyema tukatambua via vya uzazi na jinsi hukumbana na hali hiyo hiyo katika uumbaji na kuzaliwa, hivyo basi tunapaswa kuwatendea kama binadamu na ikiwa tunawatendea kama  binadamu lazima wawe na haki na majukumu yao yatambulike bila unyanyapaa.” Amesema Bi. John.

Nae Dk. Edna Majaliwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili amesema kuwa kwa mwezi huwa wanazaliwa wastani wa watoto 30, wenye hali kama hiyo hivyo basi wao wakiwa na jopo la madaktari huwa wanakutana na kujua namna ya kuweza kutatua changamoto.

“Hii ni hali ambayo mtoto huwa anazaliwa nayo, hivyo basi ikitokea amezaliwa hivyo sisi tunakutana na jopo la madaktari tunafanya vipimo na kuona ni jinsia ipi ambayo Ina nguvu zaidi hivyo tunawashirikisha wazazi pamoja na ndugu basi tunatatua hiyo changamoto.

Watoto wengine huwa tunawaacha wakuwe ili tujue jinsi gani iliyozidi ndio tunatatua changamoto, alimaliza kumesema Dk. Majaliwa.



Post a Comment

0 Comments