Ticker

6/recent/ticker-posts

WHO:hospitali ya Al Shifa katika mji wa Gaza haiwezi tena kuendesha shughuli zake



Shirika la afya duniani WHO limesema hospitali ya Al Shifa katika mji wa Gaza haiwezi tena kuendesha shughuli zake.

Maelfu ya watu wanaripotiwa kukwama ndani ya hospitali hiyo iliyokatiwa umeme kufuatia mashambulizi makali yaliyolenga eneo hilo.

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema “milio ya risasi na milipuko ya mara kwa mara” katika eneo karibu na hospitali “imezidisha hali ambayo tayari ni mbaya” na kwamba Al-Shifa “haifanyi kazi kama hospitali tena”.

Jeshi la Israel limekariri kuwa “liko tayari kusaidia” kuwahamisha watoto kadhaa wachanga walio katika mazingira magumu wanaotunzwa kwenye hospitali hiyo hadi hospitali nyingine.

Mkuu wa upasuaji wa Al-Shifa, Dkt Marwan Abu Saada, ameambia BBC kwamba mtoto wa tatu aliyezaliwa kabla ya wakati amefariki kwa sababu ya ukosefu wa umeme.



Post a Comment

0 Comments