Ticker

6/recent/ticker-posts

Hadi kufikia sasa miili iliyopatikana ni 87 na yote imeshatambuliwa na Ndugu zao



Serikali ya Tanzania jana Jumapili December 10, 2023, imetoa taarifa kuhusu maendeleo ya hali baada ya maafa ya maporomoko ya tope, mawe, magogo na maji kutoka Mlima Hanang Wilayani Hanang Mkoani Manyara ambapo imesema hadi kufikia sasa miili iliyopatikana ni 87 na yote imeshatambuliwa na Ndugu zao na kuchukuliwa kwa mazishi.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dodoma, Mobhare Matinyi, amesema kwa maelekezo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali inagharamia mazishi yote na kutoa mkono wa pole wa Tsh. milioni moja kwa kila mwili ambapo kama Familia imepoteza Watu watano inapewa Tsh. milioni tano.

“Hadi sasa jumla ya majeruhi na Wagonjwa waliopokelewa tangu maafa yatokee ni 139 lakini waliopo Hospitalini hadi leo ni 30, Wagonjwa wengine wote isipokuwa wawili waliofariki wamesharuhusiwa kurejea nyumbani”



Post a Comment

0 Comments