Ticker

6/recent/ticker-posts

Kasisi wa Kikatoliki auawa kwa kuchomwa kisu katika eneo la kanisa lake



Mtu anayedaiwa kuwa muuaji aliyemchoma kisu kasisi wa Kanisa Katoliki katika jamii ndogo ya Nebraska ametambuliwa.

Kierre L. Williams, mwenye umri wa miaka 43, wa Kaunti ya Sioux, Iowa, nchini Marekani alikamatwa kwa kumuua Kasisi Stephen Gutgsell, mwenye umri wa miaka 65, wakati wa uvamizi katika kanisa la Katoliki la St. John the Baptist huko Fort Calhoun, Nebraska, polisi walisema.

Williams alishtakiwa kwa mauaji na kutumia silaha kutekeleza uhalifu,

Gutgsell, mwenye umri wa miaka 65, alipiga simu kwa namba 911 mwendo wa saa kumi na moja asubuhi, ambapo aliwaambia polisi kwamba mtu fulani alikuwa akijaribu kuingia kwenye kata hiyo.

Polisi walimkuta Gutgsell akiwa amejeruhiwa na mtu anayedaiwa kuwa mshambulizi ndani na haijulikani  sababu ya William kumuua Gutgsell.

Gutgsell alipelekwa katika hospitali ya Omaha, ambapo alifariki kutokana na majeraha yake ya kisu, maafisa wa kanisa walisema.

Mshukiwa alipelekwa katika jela ya Washington County na ofisi ya sheriff ilisema kuwa uchunguzi unaendelea.

‘Yeye si wa eneo hilo. Yeye hatoki Fort Calhoun au hata Nebraska kama tunavyojua,’ maafisa wa sheriff walisema.

Taarifa kutoka kwa kanisa la mtaa ilisema: ‘Ofisi ya Sheriff ya Jimbo la Washington inachunguza, na hakuna maelezo zaidi kwa wakati huu.’

“Tafadhali ungana na Askofu Mkuu George Lucas katika maombi ya kumpumzisha Padre Gutgsell, kwa ajili ya familia yake na jumuiya ya parokia ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji katika kipindi hiki cha majonzi,” taarifa ya kanisa hilo ilisema.



Post a Comment

0 Comments