Ticker

6/recent/ticker-posts

Kuanza kupata hedhi kabla ya umri wa miaka 13 na hatari ya kupata Ugonjwa wa Kisukari



Tafiti: Kuanza kupata hedhi kabla ya umri wa miaka 13 kunaripotiwa kuhusishwa na hatari kubwa ya kupata kisukari cha aina ya 2(type 2 diabetes) baadaye maishani.

Utafiti huo uliochapishwa leo katika jarida la “BMJ Nutrition Prevention & Health” unaripoti kwamba mizunguko ya hedhi kuanza katika umri mdogo pia ilihusishwa na ongezeko la hatari ya kupata kiharusi kabla ya umri wa miaka 65, hasa kwa wanawake waliokuwa wanapata hedhi kabla ya umri wa miaka 10.

“Umri wa awali katika hedhi [kuanza kwa hedhi] unaweza kuwa mojawapo ya viashirio vya maisha ya badae ikiwemo kupata ugonjwa wa moyo na mishipa ya damu kwa wanawake mapema Zaidi.

Ufafanuzi Zaidi ni kwamba wanawake wanaoanza kupata hedhi katika umri mdogo huathiriwa na estrogen kwa muda mrefu, na hedhi ya mapema imehusishwa na viwango vya juu vya estrojeni,” waandishi wa utafiti huo waliandika.

#TafitiMpya



Post a Comment

0 Comments