Ticker

6/recent/ticker-posts

Magonjwa yote ya kinywa yanazuilika na kwa kiasi fulani, yanatibika



Kuna uhusiano kati ya kinywa na mifumo tofauti ya mwili ikiwemo mfumo wa kinga mwilini, na hii inaonyesha umuhimu wa kuwa na kinga ya mwili imara ili kuzuia Ugonjwa wa meno.

Kinywa chako huweza kushambuliwa na viini mbali mbali vya magonjwa ikiwemo bacteria,Fangasi, Virusi n.k

Lakini pia ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini ikiwemo Vitamins, huweza kuathiri afya ya kinywa,Meno,Lips za Mdomo,ngozi ya ndani na nje ya mdomo n.k.

“Magonjwa yote ya kinywa yanazuilika na kwa kiasi fulani, yanatibika kabsa – isipokuwa saratani hasa ikiwa kwenye hatua za mwishoni, ambayo hii ni hadithi nyingine tofauti kabisa,

Ni muhimu watu kufanya checkup ya kinywa mara kwa mara ili kuhakikisha afya ya kinywa wakati wote, Watu wanaweza kuwa na daktari wa meno wanayemwamini ambaye ana uwezo wa kuwafanyia checkup,kuwatibu na kuwapa njia sahihi za kuzingatia kama kinga dhidi ya magonjwa yote ya kinywa.

“Hiyo ni mojawapo ya njia ambayo itakusaidia kulinda afya ya kinywa, Na pia unganisha daktari wa meno na wa magonjwa mengine kwa ukaribu zaidi, ili tunapomtembelea daktari wetu wa meno, wasiangalie meno yetu tu bali waone mwili mzima kama mfumo; na kuoanisha dalili.”

Mfano mzuri ni katika utunzaji wa ujauzito: kutokana na mabadiliko ya vichocheo mwilini au homoni yanayotokea wakati wa ujauzito, bakteria wa kinywani wanaweza kupata nguvu na kumuweka mama na mtoto katika hatari zaidi.

“Hii inaweza kuongeza hatari ya mtoto kuzaliwa kabla ya wakati na kuzaliwa akiwa na uzito wa chini, ndiyo maana ni hatua muhimu kuzungumza na mama na kumpa huduma ya kutosha.”



Post a Comment

0 Comments