Ticker

6/recent/ticker-posts

Raisi Dkt. Samia Suluhu akiwa amembeba mtoto Wina Joseph mmoja wa waathirika wa mafuriko Hanang



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amembeba mtoto Wina Joseph mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 8 ambaye pia yeye na mama yake ni waathirika wa mafuriko yaliyotokea Katesh Wilayani Hanang

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewajulia hali majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Tumaini Wilayani Hanang kwa kuwapa pole pamoja na kuwatakia afya njema.

Rais Dkt. Samia ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel pamoja na Viongozi na Watendaji wengine.

Aidha Mhe. Rais Dkt. Samia amewapongeza wataalam wa afya kwa kuwahudumia vyema majeruhi pamoja na wagonjww wanaofika Hospitalini kwa ajili ya kupata matibabu.

“Madhara haya yaliyotokana na janga hilo [maporomoko Hanang] hadi sasa yamesababisha vifo 76 mpaka leo, majeruhi 117 na kaya 1,150 zenye wakazi wapatao 5,600 zimeathirika. Ekari 750 za mashamba zimeharibika, na pia kuna vifo vya mifugo” amesema Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama.



Post a Comment

0 Comments