Sababu za kuwa na Uchovu Muda wote

Sababu za kuwa na Uchovu Muda wote

Je,unahisi uchovu muda wote? bila kujali umefanya kazi ngumu au la?, Shida hii ni dalili ya nini mwilini? Soma hapa kupata majibu ya Maswali haya;

Kwenye Afya kuna nguzo tatu muhimu ambazo watu wengi hawazizingatii, nguzo hizo ni;

  1. Kulala vizuri(Sleep)
  2. Kula mlo wenye afya(Balance diet)
  3. Kufanya Mazoezi(Exercise)

Kama unatatizo la Kupata Uchovu muda wote, jitahidi kupata muda wa kutosha wa kulala,kula vizuri na fanya Mazoezi ya mwili,

Mtu mzima anashauriwa kulala Muda wa Masaa 7,8, mpaka 9, Lakini pia kula mlo kamili wenye matunda pamoja na mboga za majani. Na hakikisha unapata muda wa kufanya mazoezi ya mwili,

Pia ni muhimu sana kunywa maji ya Kutosha kila siku, maji huweza kusaidia kuondoa uchovu wa mwili.

Ikiwa umezingatia mambo yote hayo,bado unapata tatizo la Uchovu muda wote,inawezekana kuna tatizo la kiafya, na baadhi ya Matatizo haya huweza kuwa Sababu;

– Kupata Maambukizi kwenye njia ya Mkojo au Urinary tract Infections(U.T.I),

Moja ya sababu kubwa ya kupata uchovu wa mwili kwa watu wengi ni kupata maambukizi kwenye njia ya Mkojo au UTI.

– Tatizo la Upungufu wa damu mwilini(Anemia)

Watu wenye tatizo la Upungufu wa damu mwilini hasa upungufu ambao chanzo chake ni ukosefu wa madini chuma yaani “Iron-deficiency” anemia, hupata sana tatizo la mwili kuchoka sana.

watu hawa huweza kupata dalili kama vile;

  • Mwili kuchoka kupita kiasi
  • Kupata kizunguzungu hasa wakati wa kusimama
  • Mapigo ya moyo kwenda mbio n.k

– Ugonjwa wa kisukari(Diabetes)

Madaktari hawajui ni kwa nini hasa kisukari huwafanya watu wachoke sana. Ingawa Sababu mojawapo inayowezekana ni kwamba mwili wako hutumia nishati nyingi kushughulikia mabadiliko yako ya mara kwa mara katika viwango vya sukari kwenye damu.

Uchovu ni mojawapo ya dalili za kawaida za ugonjwa wa kisukari. Ina ishara nyingine, pia. Unaweza kuhisi kiu na kukojoa mara kwa mara.

– Matatizo ya tezi la Thyroid

Hili ni tezi lililopo eneo la shingoni, tezi hili hutengeneza vichocheo(hormones) ambazo husaidia kudhibiti jinsi mwili wako unavyotumia nishati.

Ikiwa tezi hili halifanyi kazi vizuri(underactive thyroid), unaweza kupata tatizo la mwili kuchoka sana.

– Magonjwa ya Moyo(Heart Diseases)

Mwili kuchoka kupita kiasi ni mojawapo ya dalili ambayo hutokea sana kwa watu wenye tatizo la Moyo kushindwa kufanya kazi(congestive heart failure).

Na uchovu huu hutokea Zaidi pale ambapo Moyo unashindwa kusukuma damu vizuri kama kawaida.

– Tatizo la kukosa hewa na kupumua kwa shida wakati umelala(Sleep Apnea)

Hali hii huweza kukusababishia uchovu sana wa Mwili.

– Tatizo la Depression

Tatizo hili huweza kuathiri kemikali zinazohitajika ili ubongo ufanye kazi vizuri,

Mojawapo ni serotonin, ambayo husaidia kudhibiti shughuli mbali mbali ndani ya mwili.

Mtu mwenye tatizo la Depression huweza kuhisi uchovu wakati wote, na pia huweza kukosa usingizi.

Ongea na daktari wako ikiwa unafikiri una huzuni. Tiba ya mazungumzo na dawa inaweza kusaidia.

– Kuwa na Ujauzito/Mimba

Pia wakina mama Wajawazito hukumbana na tatizo la uchovu wa mwili mara kwa mara.

Hizo ndyo baadhi ya Sababu za kuwa na Uchovu Muda wote….!!!!

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!