Ticker

6/recent/ticker-posts

Tabasamu larudi kwa mama aliyekatwa mikono na mtalaka wake



Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imerejesha tabasamu kwa Mkazi wa Mtwara Bi. Fadina Namponda aliyekatwa mikono miwili kwa panga na mtalaka wake baada ya kumtengenezea viungo saidizi vitavyomsaidia kufanya shughuli zake za kimaendeleo.

Akizungumza katika mahojiano na MOI TV jana tarehe Novemba 16, 2023 Fadina ameushukuru Uongozi, madaktari na watumishi wote wa taasisi ya MOI kwa jitihadi na ukarimu waliomuonesha katika safari yake ya matibabu katika taasisi hiyo.

“Nimefurahishwa na matibabu ya MOI kwasababu madaktari wake wakarimu yaani sijaona adha yeyote tangia nimeingia MOI mpaka leo hii nakabidhiwa viungo saidizi vitavyonisaidia katika usafi binafsi ambao ulikuwa ni kilio changu kizito na itanisaidia pia kufanya shughuli nyingine ndogo ndogo na utanipa wepesi wa kufanya shughuli za maendeleo” alisema Namponda

Naye Mtaalam wa viungo saidizi MOI Bi. Leah Mamseru alisema kwa sasa Fadina anaweza kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kunywa maji, kubeba vikapu anapoenda sokoni, kuvua na kuvaa nguo pamoja na shughuli nyingine ndogo ndogo.



Post a Comment

0 Comments