Ticker

6/recent/ticker-posts

Tuhuma za utakatishaji fedha: Ninakufa kwa saratani, niruhusu nirudi nyumbani- Diezani amsihi Rais Tinubu



Tuhuma za utakatishaji fedha: Ninakufa kwa saratani, niruhusu nirudi nyumbani- Diezani amsihi Rais Tinubu.

NIGERIA: Waziri wa zamani wa mafuta ya petroli wakati wa utawala wa Rais Goodluck Ebele Jonathan, ambaye alikimbilia Uingereza kwa hofu ya EFCC Diezani Alison Maduekwe sasa ameiomba serikali ya Nigeria kumhurumia.

Taarifa iliyotolewa na EFCC inasema Bi Diezani, ambaye inasemekana anaugua hatua ya pili ya saratani, anamwomba rais Bola Ahmed Tinubu amruhusu kurejea Nigeria kukiri ubadhirifu wake akiwa madarakani.

Bi Diezani alikuwa akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari mjini London baada ya ziara ya matibabu. Waziri huyo wa zamani wa Petroli, ambaye alishutumiwa kwa kuiba pesa za Nigeria, kiasi cha mabilioni ya dola, alifichua kuwa sasa yuko tayari kufunguka kuhusu pesa anazodaiwa kuzifuja akiwa ofisini kama waziri wa Petroli.

‘’Mimi ni Mkristo niliyezaliwa mara ya pili na kwa sasa ninaugua saratani ya hatua ya pili, ambayo daktari wangu wa Uingereza alinishauri niendelee kutumia dawa maisha yangu yote. Ndiyo, hakuna mwanadamu mkamilifu, lakini wakati fulani, Mungu Mweza Yote huruhusu baadhi ya mambo hayo yatukie.

Nimeshitakiwa kwa ubadhirifu wakati nikiwa waziri wa petroli, ni kweli! lakini ningependa Rais Bola Ahmed Tinubu na Wanigeria wanisamehe nirudi nyumbani na kutoa mchango wangu kwa sababu maisha ni ya muda”, taarifa kutoka EFCC inasema Diezani alisema huku akitokwa na machozi.

Taarifa kutoka EFCC inasomeka zaidi;

“Mume wangu na wanafamilia yangu yote akiwemo mwanasheria wangu wa Nigeria anayeishi Uingereza walijua uhusiano wangu na Dauda Lawal Dare, gavana wa sasa wa Jimbo la Zamfara ambaye nilimkabidhi zaidi ya dola bilioni 9 kwa ajili ya ulinzi wakati akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kwanza. Nigeria PLC.

Kwa bahati mbaya, sasa imefika mahali Bwana Dauda Lawal hapokei tena simu zangu na hata alifanya kazi kwa Ushirikiano na polisi wa Uingereza kuniweka chini ya Uangalizi, inaweza kuwa kudai Pesa nilizomkabidhi nikifa” alisema.



Post a Comment

0 Comments