Ticker

6/recent/ticker-posts

Ujenzi Daraja la Sukuma lagharimu shilingi Bilioni 11.4



Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameidhinisha shilingi bilioni 11.4 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Sukuma lenye mita 70 wilayani Magu mkoani Mwanza pamoja na barabara unganishi ya kilometa 2.2, ujenzi utakaokamilika baada ya miezi 18.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo wilayani Magu mkoani Mwanza baada ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa daraja hilo kati ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na kampuni ya Mumangi Construction Ltd ambapo ujenzi huo ukikamilika utaepusha wananchi na ajali ambazo zingeweza kutokea.

Aidha, Waziri Bashungwa ametoa wito kwa waendeshaji wa vyombo vya moto kuwa makini kwenye safari zao hasa katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Kwa upande wake Mtendaji wa TANROADS Mohamed Besta amesema usanifu wa kina wa Daraja la Sukuma na barabara unganishi ulifanywa mwaka 2021/22 na kampuni ya kizalendo ya hapa nchini, na kuahidi kumsimamia mkandarasi ili likamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa.



Post a Comment

0 Comments