Ticker

6/recent/ticker-posts

Umri sahihi wa mwanaume kupata Mtoto



Umri sahihi wa mwanaume kupata Mtoto

Umri sahihi wa mwanaume kupata mtoto unaweza kutofautiana kwa kila mtu na inategemea mambo mengi, kama vile afya ya mwanaume na maisha yake.

Kwa ujumla, wanaume wengi wana uwezo wa kuzaa wakati wowote kuanzia kwenye umri wa miaka 20 hadi miaka 50. Hata hivyo, umri unavyoongezeka, inaweza kuathiri ubora wa manii na kuongeza hatari ya matatizo ya uzazi.

Wanaume wengi mara nyingi wanafikiri kwamba umri wao haujalishi linapokuja suala la kuwa na mtoto na swala la Umri ni muhimu tu kwa mama anayezaa mtoto,

Hata hivyo, idadi na ubora wa manii hupungua kwa kadri ya umri wako unavyoongezeka. Kutoka kwenye mtazamo wa kibiolojia, wataalam wanapendekeza kwamba mwanamume anafaa zaidi kuwa baba kuanzia akiwa na umri wa miaka 20 hadi 30.

Hata hivyo inawezekana kwa wanaume kuwa na mtoto hata wakiwa na umri wa miaka 50 na zaidi. Kulingana na Guinness World Records, mwanamume mzee zaidi kuwa na mtoto alikuwa na umri wa miaka 92 wakati wa kupata mtoto. Bado, watafiti wamegundua kwamba umri wa mwanamume unaweza kuathiri uwezo wa Mwanamke kupata mimba. Wanaume wenye zaidi ya umri wa miaka 40 wana uwezekano mdogo wa kupata watoto ikilinganishwa na wale wenye umri wa miaka 20 mpaka 30.

Pia tafiti zinaonyesha kadri Mwanaume anavyopata mtoto katika umri mkubwa, ndivo matatizo ya Uzazi huongezeka zaidi, ikiwemo matatizo kama vile;

  • Mimba kutoka zenyewe
  • Kuzaa mtoto mwenye uwezo mdogo wa kiakili
  • Kuzaa mtoto mwenye matatizo ya Neva
  • Kuzaa mtoto mwenye tatizo la Usonji n.k

Kwa Mujibu wa Takwimu za ncbi;

*Kwa ujumla, uwezo wa kuzaa huanza kupungua kwa wanaume wanapokuwa na umri wa miaka 40, na Uzazi hupungua hadi asilimia 23% kwa kila mwaka kwa wanaume wenye umri wa kuanzia miaka 39,

Utafiti mmoja ulipendekeza kuwa kupata mimba katika kipindi cha miezi 12 kulikuwa na uwezekano mdogo wa asilimia 30% kwa wanaume waliokuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 ikilinganishwa na wanaume waliokuwa chini ya miaka 30.

Utafiti mwingine wa intrauterine insemination artificial insemination uligundua kwamba baada ya mizunguko sita, wanaume waliokuwa na umri wa miaka 35 au chini ya hapo walikuwa na kiwango cha uzazi cha asilimia 52%, ambapo wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 35 walikuwa na kiwango cha uzazi cha asilimia 25%.

Baada ya mizunguko sita, wanaume wenye umri wa ≥ miaka 35 walikuwa na viwango vya uzazi vya 25% ikilinganishwa na viwango vya uzazi vya 52% kwa wanaume wenye umri wa chini ya miaka 35, ikiwakilisha kupungua kwa 52% kwenye kiwango cha uzazi.

Utafiti Mwingine pia uligundua kuwa uwezo wa manii kusafiri(motility rate) ulibadilika kulingana na umri,

Motility rate huhusisha Uhamaji wa manii au uwezo wa manii kusafiri ni jinsi manii zinavyoogelea vizuri. Sasa basi,utafiti huu ulionyesha Uhamaji wa mbegu ulikuwa bora zaidi kabla ya umri wa miaka 25 na chini kabisa baada ya miaka 55.

Kwa kweli, wakati wa kulinganisha idadi ya manii  “zinazoogelea vizuri” kwa wanaume kati ya umri wa miaka 30 hadi 35 na wanaume zaidi ya umri wa miaka 55, motility ya manii ilipungua kwa asilimia 54% kadri umri ulivyoongezeka.

Ni muhimu kwa wanaume kuzingatia afya zao, lishe bora, kuepuka mambo kama vile uvutaji sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi, na kushauriana na wataalamu wa afya wanapopanga kuanza familia au wanapokuwa na wasiwasi kuhusu uzazi wao.

Hatari Za Ujauzito kulingana na Umri

Kwa Sababu ya mabadiliko yanayotokea kwenye yai pamoja na mbegu za kiume kadri umri unavyokuwa mkubwa, watoto wanaozaliwa na wazazi wenye umri mkubwa wapo kwenye hatari zaidi ya kupata matatizo(birth defects and genetic abnormalities).

Hatari ya kupata watoto wenye matatizo ya kiakili ikiwemo tatizo la Usonji(Autism spectrum disorder) ni kubwa ikiwa watoto hao walizaliwa na akina Baba wenye umri wa Zaidi ya miaka 40 ikilinganishwa na wale wenye umri mdogo zaidi.

Pia inakadiriwa kuwa,hatari ya kupata mtoto mwenye tatizo la chromosomal (or genetic) abnormality ni takribani mtoto mmoja kati ya 400 kwa Wanawake wenye umri wa miaka 30, na mtoto mmoja kati 100 kwa wanawake wenye umri wa miaka 40.

Hatari za kuharibika kwa mimba na matatizo katika ujauzito na kuzaa ni kubwa zaidi kwa wanawake wakubwa kuliko kwa wanawake wadogo.

Wanawake wazee pia wana uwezekano mkubwa wa kupata kisukari wakati wa ujauzito, tatizo la placenta previa, placental abruption, kuzaa watoto waliofariki(stillbirth) na kujifungua kwa upasuaji kuliko wanawake wasio na umri mkubwa sana.



Post a Comment

0 Comments