Ticker

6/recent/ticker-posts

AFCON: Mashabiki sita wa Guinea wafariki wakati wakisherehekea kuishinda Gambia katika Kombe la Mataifa Afrika



AFCON: Mashabiki sita wa Guinea wafariki wakati wakisherehekea kwa magari na pikipiki baada ya kuishinda Gambia katika Kombe la Mataifa Afrika,

Shirikisho la Soka la Guinea limetoa wito wa utulivu baada ya wafuasi sita kufariki wakishangilia ushindi wa nchi hiyo dhidi ya Gambia katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayoendelea.

Aguibou Camara alifunga bao pekee na kuipa Guinea ushindi mwembamba wa 1-0 Ijumaa iliyopita, na kuipa nchi yake matumaini ya kutinga hatua ya mtoano ya michuano hiyo.

Ushindi huo ulipelekea mashabiki katika mji mkuu wa Guinea Conakry kujitokeza barabarani kusherehekea kwa kutumia magari na pikipiki.

Shirika la habari la Agence France Presse liliripoti kuwa watu watatu walifariki wakati magari mawili yalipogongana yakiwa katika mwendo kasi, huku wengine wakijeruhiwa katika ajali za barabarani.

Baadhi ya mashabiki waliripotiwa kusherehekea kwa kukaa kwenye boneti za magari katika mji mkuu.

Meneja wa vyombo vya habari wa Shirikisho la Soka la Guinea Amadou Makadji aliiambia BBC kwamba watu sita wamethibitishwa kufariki katika sherehe hizo.

Shirikisho la soka nchini humo FA limetoa wito kwa mashabiki kusherehekea kwa njia zinazostahili ili kuepuka Majanga zaidi.

“Kilicho muhimu ni kwamba mashabiki wetu na umma wanasherehekea kwa mtindo wa kipekee,” meneja wa vyombo vya habari wa Feguifoot Amadou Makadji aliiambia BBC Sport Africa.

“Lazima wawe waangalifu sana ili wasijiweke hatarini kwa sababu lengo la soka ni kuleta furaha na sio kuacha familia zikiwa zimefiwa.

‘Hatupendi vifo vitokee, hivyo tunatoa wito kwa kila mtu kusherehekea bali ajitunze ili asipate chochote kibaya.

‘Guinea ni nchi ambayo watu wanapenda sana mpira wa miguu na wana uzoefu wa mpira wa miguu kama kwingineko duniani.’

Gwiji wa Guinea Pascal Feindouno, ambaye aliisaidia timu ya taifa kufika robo fainali tatu mfululizo kati ya 2004 na 2008, alijiunga na maombi hayo ya utulivu.

Feindouno alidai kuwa taarifa za vifo vya mashabiki zinaweza kuiyumbisha timu hiyo na kuwataka wananchi ‘kuunga mkono nchi lakini wasifanye lolote la kuuana wenyewe kwa wenyewe’.



Post a Comment

0 Comments