Ticker

6/recent/ticker-posts

Bacteria wanaosababisha vidonda vya tumbo



Bacteria wanaosababisha vidonda vya tumbo

Vidonda vya tumbo kwa kawaida husababishwa na maambukizi ya bacteria wanaojulikana kama Helicobacter pylori (H. pylori) bacteria, au matumizi yaliyokithiri ya dawa jamii ya anti-inflammatory medicines (NSAIDs) kama vile ibuprofen and aspirin.

Vitu hivi vina uwezo wa kuvunja Ulinzi wa tumbo dhidi ya Tindikali(Acid) ambayo huzalishwa kwa Lengo la kumeng’enya chakula,

Hali hii hupelekea kuta za tumbo kuharibiwa na kutengeneza vidonda vya Tumbo(Stomach Ulcers).

Maambukizi ya bacteria wa Helicobacter pylori (H. pylori) hutokea wakati bacteria hawa wa Helicobacter pylori (H. pylori) wanapoweza kushambulia eneo la tumbo, na mara nyingi hutokea hata Mtu akiwa katika umri mdogo(childhood).

Maambukizi ya H. Pylori ambayo ni chanzo kikubwa cha Vidonda vya tumbo, huweza kutokea kwa Zaidi ya Nusu ya Watu Duniani,

Ingawa watu wengi hawajui kwamba wana bacteria wa H. Pylori kwa Sababu hawaugui chochote,

Baada ya kuanza kupata dalili na Ishara za Vidonda vya tumbo, ndipo wataalam wa afya hufanya vipimo vya maambukizi ya H.Pylori.

Vidonda vya tumbo vinaweza kutokea kwenye kuta za tumbo ambapo tunaita peptic ulcer(gastric ulcer), au vitokee kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ambapo hapa tunaita(duodenal ulcer).

 HELICOBACTER PYLORI

• • • • • •

FAHAMU KUHUSU BACTERIA ANAYESABABISHA VIDONDA VYA TUMBO Maarufu kama Helicobacter Pylori

Helicobacter Pylori ni Bacteria ambaye huweza kusababisha matatizo mbali mbali kwenye mwili wa Binadamu ikiwa ni pamoja na tatizo la Vidonda vya Tumbo au Peptic Ulcers.

Maambukizi ya Bacteria HELICOBACTER PYLORI huweza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia njia ya Mate,matapishi,Kinyesi n.k

DALILI ZA MAAMBUKIZI YA HELICOBACTER PYLORI

– Bacteria huyu huanza kushambulia watoto wadogo na Watu wengi hawaonyeshi dalili yoyote baada ya maambukizi,

Dalili za Maambukizi ya H.Pylori ni pamoja na;

• Mtu kupata maumivu makali ya tumbo hasa akiwa na Njaa

•  Kuhisi hali ya kuungua tumboni

• Kuhisi kichefuchefu na kutapika mara kwa mara

• Hamu ya chakula kupotea

• Tumbo kujaa gesi mara kwa mara

• Uzito wa mwili kupungua kwa kasi

N.k

UKIWA NA DALILI HIZI HAPA UNATAKIWA KUPATA TIBA MAPEMA

✓ Maumivu makali sana ya tumbo mpaka unashindwa kufanya chochote au mwili kukosa nguvu

✓ Kushindwa kumeza kitu chochote

✓ Kujisaidia kinyesi kimechanganyika na Damu

✓ Kutapika matapishi ambayo yamechanganyika na Damu

MADHARA YA MASHAMBULIZI YA HELICOBACTER PYLORI

~ Mtu kupata vidonda vya tumbo au Peptic Ulcers

~ Kuvimba kwa kuta za tumboni

~ Kupata Kansa ya tumbo

MATIBABU YA MASHAMBULIZI YA HELICOBACTER PYLORI

• Tatizo hili hutibiwa kwa Dawa mbali mbali kama vile;

– Dawa jamii ya PROTON PUMP INHIBITORS ambazo huzuia uzalishaji wa Acid tumboni kama vile; OMEPRAZOLE, ESOMEPRAZOLE, PANTOPRAZOLE n.k

– Dawa jamii ya HISTAMINE BLOCKERS kama CIMETIDINE n.k

Kujua zaidi Kuhusu VIDONDA VYA TUMBO soma hapa

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments