Ticker

6/recent/ticker-posts

Chanjo ya HPV ni nini, Soma Zaidi kuhusu Chanjo ya HPV



Chanjo ya HPV ni nini, Soma Zaidi kuhusu Chanjo ya HPV

Ni kwanini Watu Zaidi huendelea kusisitizwa kupata Chanjo ya HPV, je Chanjo ya HPV ni nini? Soma Zaidi hapa.!!

HPV- ni kifupi cha Maneno “Human Papilloma Virus”

Ambapo hapa tunaelezea Kirusi kinachosababisha Saratani ya shingo ya Kizazi(Cervical cancer) kwa kiwango kikubwa.

Chanjo ya HPV:

Kulingana na Utafiti,Chanjo ya HPV inaweza kupunguza visa vya saratani ya shingo ya kizazi(Cervical cancer) kwa karibu asilimia 90%.

Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO);

Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ya nne kwa wanawake duniani kote, na husababisha vifo vya zaidi ya watu 300,000 kila mwaka.

Je,Chanjo ya HPV inauwezo wa kuzuia saratani?

Chanjo ya HPV ina uwezo wa kuzuia aina tisa za HPV.

Ni pamoja na aina mbili zinazosababisha karibu visa vyote vya saratani ya shingo ya kizazi, zile zinazosababisha saratani nyingi za njia ya haja kubwa, na saratani zinyingine za sehemu za siri, kichwa na shingo.

Utafiti umeonyesha kuwa chanjo hiyo ina kinga dhidi ya maambukizi ya HPV kwa angalau miaka 10, ingawa wataalamu wanatarajia kinga hiyo kudumu kwa muda mrefu zaidi.

Utafiti unaonyesha kuwa inaweza kupunguza visa vya saratani ya shingo ya kizazi kwa karibu asilimia 90%.

Nani anaweza kupewa chanjo ya HPV?

Chanjo ya HPV inafanya kazi vizuri zaidi ikiwa wasichana na wavulana wataipata kabla ya kupata HPV.

Hii ni kwa sababu chanjo inaweza tu kuzuia maambukizi, haiwezi kuondoa virusi mwilini mara mtu anapopatwa na maambukizi.

Virusi hivyo vimeenea sana kiasi kwamba chanjo inapaswa kulenga watoto kabla ya kufanya ngono.

Chanjo hiyo inaweza kutolewa kama dozi moja au mbili, linasema shirika la afya duniani (WHO). Watu walio na mifumo ya kinga dhaifu wanapaswa kupokea dozi mbili au tatu.

Fahamu kuhusu HPV:

Kuna aina zaidi ya 100 tofauti za HPV na maambukizi hayasababishi dalili zozote – ingawa baadhi ya aina zinaweza kusababisha maumivu. Virusi hivi vinaweza kuonekana kwenye mkono wako, mguu, sehemu za siri au ndani ya mdomo wako.

Watu wengi, hata hivyo, hawatajua wameambukizwa na miili yao itaondoa virusi bila matibabu.

Aina za hatari za HPV, kwa upande mwingine, Zinaweza kusababisha ukuaji wa tishu zisizo za kawaida ambazo zinaweza kusababisha saratani.

Ni rahisi sana kupata Virusi vya HPV kwa kuwa vinaambukizwa sana na kwa haraka Zaidi, na huenezwa kwa mgusano wa karibu wa ngozi.

Asilimia 80% ya watu huambukizwa virusi vya HPV wakiwa na umri wa miaka 25.

Katika visa vingi watu huambukizwa kwa miezi 18 hadi miaka miwili.

Mara nyingi HPV huambukizwa wakati wa kufanya ngono, ikiwa ni pamoja na mgusano wakati wa tendo la Ndoa.

Je, chanjo ya HPV imeenea kwa kiasi gani duniani kote?

Ethiopia ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazotoa chanjo ya HPV

Kiwango cha juu cha maambukizi ya HPV kwenye kizazi miongoni mwa wanawake kinapatikana katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara (24%), ikifuatiwa na Amerika ya Kusini na Caribbean (16%), Ulaya Mashariki (14%), na Kusini Mashariki mwa Asia (14%), inasema WHO.

Uchunguzi mdogo, ufikiaji mdogo wa huduma za matibabu na kusita kwa chanjo vyote vinachangia hili.

Rwanda ilikuwa moja ya nchi za kwanza barani Afrika kuanzisha kampeni ya chanjo. Ilianzisha mpango huo mwaka 2011 wa kuwawezesha wasichana kupata chanjo mapema na kuanzisha uchunguzi wa shingo ya kizazi kwa wanawake.

Katika mwaka wa kwanza iliwafikia wasichana tisa kati ya 10 wanaostahili kupata chanjo hiyo, matokeo ambayo wataalamu wanayataja kama mfano kwa nchi nyingine.

Ingawa chanjo hiyo inaonekana kupunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kupata saratani ya shingo ya kizazi, sio kinga dhidi ya aina zote za HPV.

Hivyo ni muhimu kwa wanawake pia kufanya kipimo cha uchunguzi wa saratani ya shingo ya uzazi ( Papsmears ) mara kwa mara wanapofikia umri wa miaka 25.

Soma Zaidi hapa: Kuhusu Chanjo ya HPV



Post a Comment

0 Comments