Ticker

6/recent/ticker-posts

Habari na hoja mchanganyiko kuhusu Mastaa-Mtoto wa Snoop Dogg kugundulika kiharusi



habari na hoja mchanganyiko kuhusu Mastaa-Mtoto wa Snoop Dogg kugundulika kiharusi

Mtoto wa Snoop Dogg,Cori Broadus apata kiharusi

Cori Broadus, binti wa Mwanamuziki(rapa) Snoop Dogg, amesema aliangua kilio wakati madaktari walipomwambia kuwa alikuwa na “kiharusi ” akiwa na umri wa miaka 24.

Broadus alisambaza habari hiyo pamoja na picha zake kwa wafuasi wake 657,000 katika mtandao wa Instagram siku ya Alhamisi akiwa amelazwa kwenye kitanda cha hospitali,

Alitoa maoni: “Nilipata kiharusi kikali mapema leo. Nilianza kuangua kilio waliponiambia.

“Nina umri wa miaka 24 tu. Nilifanya nini katika siku zangu zilizopita ili kustahili haya yote?”

Madaktari wakati mwingine hutaja kiharusi kama mshtuko wa moyo kwa ubongo.

Inatokea wakati damu inaposhindwa kufika katika ubongo.

Akijibu marafiki waliomtumia salamu za heri kwenye Instagram, Broadus alichapisha: “Nawapenda nawapenda.”

Mwanamuziki na mjasiriamali Snoop Dogg, ambaye jina lake halisi ni Calvin Cordozar Broadus Jr, pia ana watoto wawili, Corde na Cordell, na mkewe Shante.

Rapa huyo alijipatia umaarufu mkubwa kufuatia kutolewa kwa albamu yake ya kwanza ya mwaka 1993, Doggystyle – iliyotayarishwa na Dr Dre.

Chanzo: Bbc



Post a Comment

0 Comments