Ticker

6/recent/ticker-posts

kupata mimba haraka,awapa Mimba wanawake watano kwa mpigo



kupata mimba haraka,awapa Mimba wanawake watano kwa mpigo

Marekani. Katika hali ya kushangaza, mwanamuziki nchini Marekani, Zeddy Will amewafanyia sherehe wanawake watano aliowapa ujauzito kwa mpigo.

Sherehe hiyo kabla ya mtoto kuzaliwa (Baby Shower) imegeuka gumzo kwenye mitandao ya kijamii, wengi wakihoji ni njia gani ameitumia kuwafanya wanawake hao kuelewana na kukubali kushiriki sherehe hiyo ya pamoja.

Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Mail, tukio hilo lilionekana kwa mara ya kwanza kupita mtandao wa kijamii wa Tiktok ambako picha ya mjongeo (video) ilichapishwa na mmoja wa wanawake hao.

Lizzy Ashleigh, ndiye alichapisha video hiyo huku  akiweka wazi juu ya sherehe hiyo iliyofanyika Januari 14, 2024.

Mwaliko wa sherehe hiyo ulikuwa umeambatanishwa na maneno yasemayo, “Welcome little Zeddy Wills 1-5.”

Wanawake wengine waliopewa ujauzito na mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 22 ni Bonnie B, Jylene Vila, Kay Marie, na Iyanla Kalifa Galletti.

Akizungumzia tukio hilo kupitia chapisho lake, Ashleigh aliambatanisha ujumbe unaosema “Nadhani sasa ni wake wenza.”

Picha hizo za sherehe ya kujiandaa kuwapokea watoto zilikuwa zimepambwa na nyuso za tabasamu, huku video za wanawake hao zilionyesha wakifurahi na kucheza.

Zeddy, baba mtarajiwa wa watoto hao watano alionekana katika moja ya picha akiwa katikati ya wanawake hao, Ashleigh alimtambulisha.

Mwanamke huyo amesema wote kwa pamoja wamekubali kuelewana kwa faida ya watoto wao ambao watakuwa ndani ya familia kubwa.



Post a Comment

0 Comments