Ticker

6/recent/ticker-posts

kuzaa kwa upasuaji mwisho mara ngapi



kuzaa kwa upasuaji mwisho mara ngapi

Kuzaa kwa Upasuaji, kwa miaka ya hivi karibuni idadi ya wanawake wanaojifungua kwa njia ya upasuaji(C-Sections) inazidi kuongezeka,

Hizi hapa ni baadhi ya Sababu za Wanawake wengi kujifungua kwa njia ya upasuaji. Soma Zaidi Hapa;

Ila katika Makala ya Leo,tunajibu Swali la”kuzaa kwa upasuaji mwisho mara ngapi?”

Linapokuja Suala la Idadi au ni mara ngapi ufanyiwe upasuaji wakati wa kujifungua, hakuna jibu la moja kwa moja kwani hutegemea na sababu nyingi ikiwemo; afya ya mama kwa jumla pamoja na Mtoto aliyetumboni.

Kuna watu hufanya upasuaji hata Zaidi ya Mara 3 lakini hawapati tatizo lolote na wengine hufanya upasuaji mara moja tu na kuanza kupata matatizo hapo hapo.

Mfano; Kwa Mujibu wa chapisho moja kutoka Healthlines linasema nanukuu;

“There are some people who have had six or seven C-sections without any issues, and others with only one C-section whose next pregnancy is associated with a very difficult problem such as placenta accreta spectrum disorder, or a horrible adhesions (things stuck together),”

KUMBUKA; INGAWA, Wataalam wengi wa afya hushauri usifanye Upasuaji wa kujifungua Zaidi ya Mara tatu(3).

Likiwemo chapisho moja lililoandikwa na Mayo clinic;

“Mayo Clinic says TOLAC isn’t recommended after three or more prior C-sections”.

Hatari Za Kufanya Upasuaji wa Kujifungua Mara Nyingi(C-Sections)

Haya hapa ni madhara unayoweza kukumbana nayo kwa kufanya Upasuaji wa kujifungua mara nyingi(Risks of multiple C-sections);

– Kupasuka au kuchanika kwa kizazi(uterine rupture)

– Kupata madhara kwenye kibofu cha Mkojo(bladder complications)

– Kupata matatizo kama vile; bowel adhesions or lacerations,omentum adhesions

– Matatizo kwenye mishipa ya damu(blood vessel complications)

– Kuvuja damu kupita kiasi(excessive bleeding)

– Kupata tatizo la kupungua kwa Damu

– Kuondelewa Kizazi(hysterectomy)

– Kuwa kwenye hatari Zaidi ya kupata matatizo yanayohusu kondo la nyuma(placenta), ikiwemo;

  • Tatizo la placenta accreta,
  • placenta previa,
  • Pamoja na placental abruption.

– Kuongezeka kwa Idadi ya Vifo, Ingawa kifo huweza kutokea kwa mtu yoyote anayefanyiwa upasuaji,

Baadhi ya tafiti za mwaka 2017 zilionyesha, Wanawake waliofanyiwa Upasuaji Zaidi ya Mara 3 walikuwa kwenye hatari zaidi za kupoteza maisha kutokana na Complications zinazoweza kutokea wakati wa Kujifungua kuliko wale waliofanyiwa chini ya hapo.

Kuzaa kwa upasuaji, au kujifungua kwa upasuaji (C-section), mara nyingine hutegemea hali ya kiafya ya mama na mtoto. Kwa kawaida, upasuaji huo hufanyika iwapo kuna matatizo au hatari kwa afya ya mama au mtoto wakati wa kujifungua.

Hata hivyo, idadi ya kufanyiwa Upasuaji wa kujifungua inaweza kutofautiana kulingana na mazingira na mahitaji ya kiafya ya kila mwanamke. Ni muhimu kushauriana na daktari wako kwa maelezo zaidi kuhusu hali yako maalum.



Post a Comment

0 Comments